SERIKALI YA TANZANIA NA NORWAY ZASAINI MAKUBALIANO KUWEZESHA WAHANDISI WANAWAKE WANAOHITIMU VYUO VIKUU
Msajili wa Wahandisi (ERB) Eng. Steven Mlote akielezea mafanikio yaliyopatikana tangu kuanza kwa Ushirikiano katika masuala ya Uhandisi kati ya ERB na Serikali ya Norway.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akijadiliana jambo na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne –Marie Kaarstad wakati wa kusaini Makubaliano ya Awali ya Programu ya kuwasaidia na kuwaendeleza Wahandisi wanawake walioko vyuoni yenye lengo la kuongeza idadi ya Wahandisi waliosajiliwa kwa ngazi ya Ushauri jana jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Tone Skogen (Katikati) kuhusu Mafanikio wanayoyapata Wahandisi Wanawake wa Tanzania kutokana na msaada wa Mafunzo ya kuwasaidia na kuwaendeleza Wahandisi wanawake walioko vyuoni kutoka Serikali ya Norway
Mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi nchini Prof. Ninatubu Lema (kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Tone Skogen (kushoto) wakisaini Makubaliano ya Awali ya Programu ya kuwasaidia na kuwaendeleza Wahandisi wanawake walioko vyuoni yenye lengo la kuongeza idadi ya Wahandisi waliosajiliwa kwa ngazi ya Ushauri.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi nchini Prof. Ninatubu Lema (kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Tone Skogen (kushoto) wakibadilishana Hati za Makubaliano ya Awali ya Programu ya kuwasaidia na kuwaendeleza Wahandisi wanawake walioko vyuoni yenye lengo la kuongeza idadi ya Wahandisi waliosajiliwa kwa ngazi ya Ushauri jana jijini Dar es salaam
Comments
Post a Comment