Posts

HOT NEWS.....MADUKA YAVUNJWA IRINGA USIKU WA LEO

Image
Wananchi wakitazama Stationery ya Nyigi iliyopo eneo la jengo la Masiti Eso ambayo imevunjwa na wezi Mmiliki wa duka la Ferick Urembo akiangua kilio kwa uchungu baada ya kukuta duka lake limevunjwa na kuibwa mali mbali mbali asubuhi hii. Wananchi wa Manispaa ya Iringa wakitazama duka la Ferick Urembo ambalo limevunjwa usiku wa leo . Wakati maandalizi ya sikuu kuu za Krismas na mwaka mpya yakianza taratibu ,watu wanaosadikika kuwa ni wezi nao wameanza kufanya maandalizi ya funga mwaka baada ya usiku wa leo kuvunja maduka mawili eneo la Eso katika Manispaa ya Iringa na kuiba mali mbali mbali. Maduka ambayo yamevunja usiku wa leo ni pamoja na duka la Ferick Urembo lililopo eneo la Natioanl katika majengo ya Bakwata , na Nyigu Stationery iliyopo eneo la jengo la Masiti Eso. Baadhi ya wamiliki wa maduka hayo wamesema kuwa maeneo yao yamekuwa yakilindwa na makampuni ya ulinzi na hadi sasa eneo la tu

Polisi wazuia maandamano

Image
*Wahofia uvunjifu amani, yalipangwa kufanyika J'mosi *Wanaharakati kutafuta njia nyingine kufikisha ujumbe *IGP Mwema asisitiza jeshi hilo halina nia mbaya SIKU moja baada ya wanaharakati kutoka asasi za kiraia zaidi ya 180, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) na Jukwaa la Katiba Tanzania kutangaza kufanya maandamano ya amani nchi nzima Novemba 26 mwaka huu, Jeshi la Polisi nchini limeyazuia kutokana na hofu ya kuvunjika kwa amani. Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, kwa vyombo vya habari, ilisema kutokana na mchakato unaoendelea wa kupitishwa kwa Muswaada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya nchini, amekuwa akipokea maombi ya kufanya maandamano kutoka taasisi mbalimbali nchi nzima yakiwa na malengo tofauti. Alisema malengo hayo ni pamoja na kupinga muswaada huo na mengine yakiunga mkono jambo linaloashiria kuleta migongano na hatimaye kusababisha uvunjifu wa amani. Alizitaja taasisi zil

KUTOKA SAUT: SHIRIKA LA KUTETEA HAKI ZA ALBINO (UTSS) LAFANYA KONGAMANO LA KUELIMISHA JAMII JUU YA VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA ALBINO

Image
Shirika lisilo la kiserikali UNDER THE SAME SUN (UTSS) linalojishughulisha na kutetea, kuelimisha jamii juu ya vitendo vya ukatili kwa watu weye ulemavu wa ngozi (ALBINO) leo limefanya kongamano pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino juu ya jinsi gani jamii inaweza kukomesha vitendo vya ukatili kwa Albino hapa nchini. Akizungumza na waandishi wa Habari Mtendaji mkuu wa idara ya habari na uhusiano wa kimataifa wa shirika hilo Mrs. Vicky A. Ntetema alisema kuwa jamii kwa ujumla inatakiwa kuungana katika kukomesha swala zima la ukatili dhidi ya vitendo vya ukatili kwa walemavu wa ngozi hapa nchini, huku akiitaka serikali kuongeza ulinzi kwa watu wenye ulemavu kwani vitendo vya ukatili vimekuwa vikiripotiwa kila siku kutokea hivyo ni dhahiri usalama wa watu wenye ulemavu wa ngozi ni mdogo. Akizungumzia swala la Waganga wa Kienyeji kama chanzo cha ukatili kwa Albino alisema ” Sioni hatua zinazochukuliwa na serikali juu ya kufungia leseni zinazotolew

Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka Atembelea Sinza Jijini Dar es Salaam na Kugundua Uuzaji Wa Maeneo Ya Wazi

Image
Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka akiongea na mkazi wa Sinza Ndahani Yohana ambaye amenunua eneo la wazi kwa utapeli kwa shilingi milioni 500 wiki mbili zilizopita, ambapo ramani halisi inaonyesha eneo hilo ni la wazi. Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi katika maeneo ya Sinza E leo mchana. Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka wa pili kutoka kulia akiangalia ramani halisi inayoonyesha maeneo ya wazi wakati alipokagua maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi maeneo ya Sinza E wilaya ya Kinondoni, ambapo pia alikuwa akikagua mabango yaliyowekwa kwa ajili ya kuataarifu wananchi na kuwaelimisha maeneo ambayo ramani inaonyesha yako wazi kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya Serikali. Diwani wa Sinza Bw. Renatus Pamba akimuonyesha Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi k

HAPPY BIRTHDAY PRO JOHN BERA

Image
WISH ALL DA BEST BRO IN UR LIFE,LIVE LONGER..................

USIKU WA PUBLIC RELATIONS MANAGERS WAFANA SANA

Image
Jana usiku ulikuwa ni usiku maalum sana kwa wanafunzi wanaosomea kozi ya Mahusiano ya umma na Masoko (PRO) wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino (SAUT)waliofanya sherehe yao pale Nyumbani hotel katika kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa Kwanza pamoja na kusherehekea ushindi wa FAWASCO (mshindi wa pili). Mgeni rasmi alikuwa ni mhadhili Emmanuel Silaa,pamoja na wageni wengine waalikwa kama Rais wa serikali ya wanafunzi (SAUTSO)Mh.Cosmas Mataba,akiambatana na waziri mkuu wake,pia na baadhi ya wahadhili kama Libelatus Chonya na Gibson.Sherehe iliambatana na burudani mbalimbali kutoka kwa wanafunzi wa PR wenye vipaji mbalimbali. Mgeni rasmi mhadhili Emmanuel Silaa alitoa nasaa zake kwa wana PR kuwa wawe na ushirikiano wa kutosha kuanzia wanafunzi wa mwaka wa kwanza mpaka wa tatu na kuheshimiana hii itapelekea kukamilisha nguzo muhimu ya kozi hii unity and solidality hata watakapomaliza masomo yao na kuelekea kazin