KUTOKA SAUT: SHIRIKA LA KUTETEA HAKI ZA ALBINO (UTSS) LAFANYA KONGAMANO LA KUELIMISHA JAMII JUU YA VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA ALBINO

Shirika lisilo la kiserikali UNDER THE SAME SUN (UTSS) linalojishughulisha na kutetea, kuelimisha jamii juu ya vitendo vya ukatili kwa watu weye ulemavu wa ngozi (ALBINO) leo limefanya kongamano pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino juu ya jinsi gani jamii inaweza kukomesha vitendo vya ukatili kwa Albino hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mtendaji mkuu wa idara ya habari na uhusiano wa kimataifa wa shirika hilo Mrs. Vicky A. Ntetema alisema kuwa jamii kwa ujumla inatakiwa kuungana katika kukomesha swala zima la ukatili dhidi ya vitendo vya ukatili kwa walemavu wa ngozi hapa nchini, huku akiitaka serikali kuongeza ulinzi kwa watu wenye ulemavu kwani vitendo vya ukatili vimekuwa vikiripotiwa kila siku kutokea hivyo ni dhahiri usalama wa watu wenye ulemavu wa ngozi ni mdogo.

Akizungumzia swala la Waganga wa Kienyeji kama chanzo cha ukatili kwa Albino alisema ” Sioni hatua zinazochukuliwa na serikali juu ya kufungia leseni zinazotolewa kwa waganga wa kienyeji kwani wamekuwa chanzo kikubwa cha kutokea matukio haya kutokana na madai ya wanaofanya vitendo hivyo vya ukatili hupata ushauri wa kuchukua viungo vya albino ili wapate kuwa matajiri”

Vicky A. Ntetema akiwasilisha mada na kutoa elimu juu ya hatua za kuchukuliwa kuweza kukomesha vitendo vya ukatili juu ya vitendo vya ukatili vinavyofanywa kwa walemavu wa ngozi hapa nchini.

Mmoja kati ya mlemavu wa ngozi ambae pia anafanya kazi na shirika hilo akisema maneno yake juu ya ukatili wanaofanyiwa na binadamu wenzao.

Viongozi wa shirika hilo wakiwa meza kuu, wa pili kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo ambae pia mlemavu wa ngozi Mr. Peter Ash.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shrika hilo Mr. Peter Ash akizungumza na wanafunzi hawapo pichani.

Baadhi ya wanafunzi wakifatilia kwa makini kongamano hilo jioni ya leo katika ukumbi wa M1. SAUT.

Sister ambae pia ni Mhadhiri wa SAUT akifatilia kwa makini kongamano hilo.

Mwanafunzi wa Shahada ya kwanza ya Mawasiliano ya Umma Ms. Lulu Sanga akichangia mawazo yake katika kongamano hilo.

Picha zilizonyeshwa ukumbini hapo kutoa hali halisi ya matatizo wanayoyapata watu wenye ulemavu wa ngozi.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA