VURUGU ZA MACHINGA ZASABABISHA MAUAJI MWANZA RISASI ZARINDIMA WATANZANIA WENYE ASILI YA ASIA WAPATA MISUKOSUKO
Magari mawili ya mfanyabiashara maarufu mkoani hapa Mukeshi vunja bei yamechomwa moto na kuteketea, vibanda kadhaa vimevunjwa, Baadhi ya bidhaa zilizopangwa nje zimeibiwa nayo matairi yamechomwa katikati ya njia panda kuingia mtaa wa Makoroboi kuelekea Soko kuu na kiunganishi cha barabara ya Lumumba Mwanza huku baadhi ya wamachinga hao wakirusha maboksi yaliyoshika moto kwenye majengo yaliyo karibu na eneo hilo kwa nia ya kuyachoma moto.
Friji ikiteketea..
Vibaka wamepora bidhaa na mali zilizokuwa nje ya Nono Super market nakisha kuchoma friji ilokuwa na vinywaji ambavyo walivinywa kabla ya kuiteketeza.
Kusanyiko la shaka-shaka.
Matairi pia yamechomwa mbele ya lango kuu la soko kuu la jijini Mwanza haliiliyopelekea kufungwa kwa soko hilo nazo biashara kusitishwa..
Wafanyabiashara wakichungulia yanayojiri nje kupitia lango kuu la soko kuu.
Kona ya kuingia barabara ya Msikiti wa Ijumaa kutokea barabara ya Nyerere risasi zimelia nao wananchi wakikimbia kujihami na mabomu ya machozi.
Market Street hakuna shughuli inayofanyika kwa sasa kwani hata vibaka wametumia mwanya huu kufanya uporaji.
Mtaa wa makoroboi kulikoanzia vurugu hakuna biashara inayofanyika maduka yote yamefungwa.
Machinga na jiwe lake mkononi tayari kulirusha..Hali imekuwa tete kwa watanzania wenye asili ya kiasia kwani imekuwa wakionekana tu wanafanyiwa kitu mbaya.
Kuvunjwa vioo kwa jengo hili la msikiti wa hindu ni moja kati ya hasara zilizojitokeza.
Mpaka sasa hivi ikiwa ni saa 6:15 barabara ya Nyerere haijatulia kwani kuna umati mkubwa wa watu eneo hili mawe yakirushwa nayo mabomu ya machozi yakisikika mitaa ya Makoroboi, Alhamini, Maketi na Msikiti wa Ijumaa kuwatawanya waandamanaji.
picha na habari ni kwa hisani ya Albert www.gsengo.blogspot.com
Comments
Post a Comment