ZAIDI YA WANAFUNZI 3000 T ARIME WANAKAA CHINI

zaidi ya wanafunzi 3000 Inakadiriwa kuwa wanakaa katika shule nne tofauti zinazozunguka mgodi wa dhahabu wa North Mara wakati wa vipindi kutokana na uhaba wa madawati katika shule zao

Hali hiyo imebanika baada ya waandishi wa habari kutembelea baadhi shule na kushuhudia sehemu ya wanafunzi wakiwa wameketi chini ya vumbi wakati vipindi vinaendelea.

aidha shule ambazo inasemekana bado asilimia kubwa ya wanafunzi wanakaa chini ni shule ya ya Nyakunguru A, Nyakunguru B, Nyamongo na Nyangoto.

katika shule ya msingi Nyakunguru A mwalimu mkuu Msaidizi wa shule hiyo Otaigo Machera amesema kuwa Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 668 ina madawati 80 ambapo Taarifa zinasema hali ni mbaya katika shule ya jirani.

AMESEMA SHULE HIYO ILIYOANZISHWA MWAKA 1958 LAKINI MPAKA SASA BADO HALI INAONEKANA KUWA MBAYA ZAIDI KATIKA SHULE HIYO AMBAYO PIA AFISA ELIMU WA WILAYA HIYO ALISOMA KATIKA SHULE HIYO.

Katika shule hizo majengo yanaonesha kuchAkAa na hayatumiki kiasi kwamba yanahatarisha maisha ya wanafunzi wanayoyatumia kama viwanja vya michezo,Hata hivyo uongozi wa kijiji cha Nyakunguru unatupiwa lawama kwa kuchelewesha kukamilika kwa ujenzi wa jengo la nyumba ya mwalimu miaka mitano sasa.

Kampuni ya African Barrick Gold ambayo inamiliki mgodi wa dhahabu wa North Mara imekuwa ikidai kutumia mamilion ya pesa kuboresha huduma za jamii katika vijiji vinavyozunguka mgodi huo.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA