ARSENAL WALAZIMISHA SARE UGENINI, BARCA YASHIKWA NYUMBANI, CHELSEA YAUA DARAJANI



BAO la Mholanzi Robin Van Persie katika dakika ya 42 usiku huu kwenye Uwanja wa Signal Iduna Park, Dortmund, Ujerumani mbele ya mashabiki 65,614 chupuchupu liipe Arsenal ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji Borussia Dortmund kama si Ivan Perisic kusawazisha dakika ya 88. Katika mchezo huo wa Kundi F, kikosi cha Gunners jana kilikuwa; Wojciech Szczesny, Bacary Sagna, Per Mertesacker, Laurent Koscielny, Kieran Gibbs, Alex Song, Mikel Arteta, Theo Walcott, Yossi Benayoun, Gervinho/Santos dk 86 na Robin Van Persie/Chamakh dk 85.
Borussia Dortmund; Roman Weidenfeller, Lukasz Piszczek, Neven Subotic, Mats Hummels, Marcel Schmelzer, Sven Bender, Sebastian Kehl/ Blaszczykowski dk 68, Mario Gotze, Shinji Kagawa/Zidan dk 85, Kevin Grosskreutz/Perisic dk 69 na Robert Lewandowski.
Aidha, mabingwa wa Ulaya wenye hadhi ya kucheza soka adimu zaidi duniani, Barcelona walilazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na AC Milan ya Italia kwenye Uwanja wa Camp Nou mjini Barcelona katika mchezo wa Kundi H.
Pato alitangulia kuifungia Milan dakika ya kwanza tu, lakini Pedro akasawazisha dakika ya 36 kabla ya mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania, David Villa kupiga la pili dakika ya 50 na Thiago Silva kusawazisha dakika ya 90.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa; Víitor Valdes, Dani Alves, Javier Mascherano, Sergio Busquets, Éric Abidal, Xavi, Seydou Keita/Carles Puyol, Andrés Iniesta/Ibrahim Afellay, Pedro, Lionel Messi na David Villa/Cesc Fàbregas.
AC Milan: Christian Abbiati, Ignazio Abate, Alessandro Nesta, Thiago Silva, Gianluca Zambrotta, Antonio Nocerino, Mark Van Bommel, Clarence Seedorf, Kevin-Prince Boateng, Pato na Antonio Cassano.
Kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, Chelsea waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani, mabao ya David Luiz dakika ya 67 na Juan Mata dakika ya 90 katika mchezo wa Kundi E.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Cech, Ivanovic, Cole, David Luiz/Alex dk 76, Bosingwa, Mikel, Malouda, Meireles/Lampard dk 65, Torres, Mata na Sturridge/Anelka dk 64.
Bayer Leverkusen; Leno, Reinartz, Omar Toprak, Kadlec, Castro, Rolfes, Bender/Balitsch dk 80, Ballack/Renato Augusto dk 66, Schurrle, Kiessling na Sam/Derdiyok dk 73.
Kwenye Uwanja wa GSP, wenyeji Apoel Nicosia waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Zenit St. Petersburg mabao yake yakitiwa kimiani na Konstantin Zyryanov dakika ya 63 na Gustavo Manduca dakika ya 73, wakati la wageni lilifungwa na Ailton Jose Almeida dakika ya 75 katika mchezo wa Kundi G.
Kwenye Uwanja wa Dragao, wenyeji FC Porto waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Shaktar Donetsk mabao yake yakitiwa kimiani na Luiz Adriano dakika ya 12 na Hulk dakika ya 28, wakati wapinzani wao walitolewa kimasomaso kwa bao la Kleber dakika ya 51 kwenye mchezo wa Kundi G.
Kwenye Uwanja wa Cristal wenyeji Genk walilazimishwa sare ya bila kufungana na Valencia katika mchezo wa Kundi E.
Bao pekee la Lucho Gonzalez dakika ya 51, lilitosha kuipa Marseille ya Ufaransa ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji Olympiacos kwenye Uwanja wa Karaiskakis katika mchezo wa Kundi F.
Kwenye Uwanja wa Sady Viktoria, wenyeji Plzen walilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na BATE, bao la wenyeji likitiwa kimiani na Marek Bakos dakika ya 45 na Renan Bressan akawasawazishia wageni dakika ya 69 katika mchezo wa Kundi H.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA