URENO KUTOKA ‘BEST LOSER’ HADI MABINGWA WA EURO 2016
Ureno wameweza kuikabili Ufaransa na kuichapa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Euro 2016 na kushinda taji lao kubwa kwa mara ya kwanza bila ya nahodha wao Cristiano Ronaldo aliyetoka mapema kipindi cha kwanza baada ya kuumia. Loser Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid alibebwa kwenye stretcher huku akibubujikwa na machozi dakika ya 25 ya mchezo dakika nane baada ya kuumia goti alipopambana na mfaransa Dimitri Payet. Ufaransa timu ambayo ilipewa nafasi kubwa ya kushinda ubingwa huo, walishindwa kupata bao kwa kutumia faida ya kukosekana kwa Ronaldo uwanjani licha ya kukaribi kupata bao dakika za lala salama kupitia kwa Andre-Pierre Gignac aliyeingia kutoka benchi ambapo shuti lake liligonga mwamba. Raphael Guerreiro alipiga mpira wa adhabu ndogo uliogonga mtambaa panya lakini sekunde chache baada ye Eder aliachia shuti la chinichini akiwa umbali wa mita 25 kutoka golini lililomshinda golikipa wa Ufaransa Hugo Lloris na ku