URENO KUTOKA ‘BEST LOSER’ HADI MABINGWA WA EURO 2016
Ureno
wameweza kuikabili Ufaransa na kuichapa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali
ya michuano ya Euro 2016 na kushinda taji lao kubwa kwa mara ya kwanza
bila ya nahodha wao Cristiano Ronaldo aliyetoka mapema kipindi cha
kwanza baada ya kuumia. Loser
Mshambuliaji
wa klabu ya Real Madrid alibebwa kwenye stretcher huku akibubujikwa na
machozi dakika ya 25 ya mchezo dakika nane baada ya kuumia goti
alipopambana na mfaransa Dimitri Payet.
Ufaransa
timu ambayo ilipewa nafasi kubwa ya kushinda ubingwa huo, walishindwa
kupata bao kwa kutumia faida ya kukosekana kwa Ronaldo uwanjani licha ya
kukaribi kupata bao dakika za lala salama kupitia kwa Andre-Pierre
Gignac aliyeingia kutoka benchi ambapo shuti lake liligonga mwamba.
Raphael
Guerreiro alipiga mpira wa adhabu ndogo uliogonga mtambaa panya lakini
sekunde chache baada ye Eder aliachia shuti la chinichini akiwa umbali
wa mita 25 kutoka golini lililomshinda golikipa wa Ufaransa Hugo Lloris
na kuzama wavuni.
Ronaldo
ambaye alikuwa akiwahamasisha wachezaji wenzake wakati wa mapumziko
kabla ya dakika 30 za nyongeza, alikuwa akitekeleza majukumu ya benchi
la ufundi sambamba na kocha Fernando Santos hasa wakati wa dakika za
mwisho na alishindwa kuzuia machozi ya furaha baada ya filimbi ya mwisho
kabla ya kunyanyua ndoo aliyoisubiri kwa muda mrefu akiwa na timu yake
ya taifa ya Ureno.
Matukio katika namba
35: Ureno wameshinda taji lao la kwanza la Ulaya baada ya mechi 35 kwenye mashindano hayo.
10: Ureno ni taifa la kumi tofauti kushinda kombe la mataifa ya Ulaya.
6: Eder
ni mchezaji wa sita kufunga goli kwenye michuano ya Ulaya akitoea benchi
anaungana na Oliver Bierhoff, Sylvain Wiltord, David Trezeguet, Juan
Mata pamoja na Fernando Torres.
3: Ureno
imekuwa nchi ya kwanza kwenye michuano ya Ulaya kucheza mechi tatu hadi
dakika 30 za nyongeza ndani ya msimu mmoja wa mashindano.
80: timu
ya taifa ya Ureno ilifanikiwa kupiga shuti lake on target dakika ya 80,
muda mrefu zaidi kwenye fainali za michuano ya Ulaya. Chanzo..shaffihdauda.com
Comments
Post a Comment