OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA YAENDELEA NA UHAKIKI WA VYAMA NCHINI

C1
Mhasibu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw.Willium Brown Nyamtiga akisisitiza jambo kwa viongozi wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Jana wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Jijini  Buguruni Dar es salaam .
Zoezi la uhakiki wa  utekelezaji wa masharti ya usajili wa Vyama va Siasa  kwa upande wa Tanzania Bara  linaendelea .Tayari  vyama 18 vimekwishakuhakikiwa. Vyama vinne vinatarajiwa  kuhakikiwa  Julai 4. Zoezi hili ni zoezi la kawaida na endelevu  ambalo hufanyika  kila mwaka ili kupima endapo vyama vya siasa   vinakidhi matakwa ya  Sheria ya usajili wa vyama vya Siasa.
Uhakiki wa Vyama vya siasa ni zoezi muhimu sana kwa sababu ni zoezi ambalo hugusa uhai wa  kila  chama cha siasa.  Kwa upande wa Tanzania Visiwani , uhakiki unatarajiwa kuanza  mara baada ya kumalizika Bara  kwa tarehe ambazo zitatangazwa baadaye.
C2
Bw.Eugene Kabendera, Katibu Mwenezi Taifa wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) akitoa taarifa  wa watumishi  kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Jijini Makumbusho Dar es salaam Juzi
C3
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Jahazi Asilia, Bw. Mbwana S. Kibanda akifafanua jambo wakati wa zoezi la uhakiki  liliofanyika  Leo katika ofisi za chama hicho zilizopo ilala Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho na kushoto ni watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
C4
Bi. Esther B.Mwanri, Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa akikagua katiba ya Chama cha Wananchi (CUF) wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo  Buguruni Malapa Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Bw. Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa uchumi na Mipango.
C5
Msajili Msaidizi wa Vyama Siasa  “Gharama za uchaguzi na Elimu kwa Umma “Bi. Piencia Kiurea akimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha United Democratic Party (UDP) Bw. Godluck Ole-Medeye wakati akitoa taarifa muhimu za chama chake katika zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Kisiasa unaoendelea Jijini Dar es Salaam.
C6
Kaimu Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party (DP) Bi. Georgia Mtikila (kushoto) akitoa taarifa za chama chake kwa Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini (kulia), Bi. Jacqueline Kilama wakati wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam Juni 28 mwaka huu.
C7
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Usajili wa vyama vya Siasa , Bw. Sisty Nyahoza (kushoto) akihakiki daftari lenye orodha ya wanachama wa Chama cha NRA ( National Reconstruction Alliance) wakati wa zoezi la kuhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa Jana Jijini Dar es Salaam.
C8
Kaimu Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party (DP) Bi. Georgia Mtikila (kushoto) akitoa taarifa za chama chake kwa Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini (kulia), Bi. Jacqueline Kilama wakati wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam Juni 28 mwaka huu.
(Picha zote na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa)

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA