CHAMA kipya cha Kutetea Haki na Maslahi ya Walimu Tanzania (CHAKAMWATA) kimesajiliwa rasmi na kupata cheti cha usajili wa kudumu kutoka Wizara ya Kazi na Ajira. Akizungumza na FikraPevu , Katibu Mkuu wa Chakamwata, Mwalimu Meshack Kapange, anasema chama hicho kipya kinaundwa na walimu nchini waliojiondoa kutoka mikononi mwa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT). Kapange amesema mchakato wake wa kukisajili chama hicho ulianza miaka minne iliyopita, hadi hivi juzi kilipopewa usajili wa kuendelea na shuhuli zake kisheria. “Ni furaha iliyoje kupata usajili huu wa chama chetu cha kutetea haki na maslahi ya walimu? Huu ni ukombozi kwa walimu wanaokatwa asilimia mbili za mishahara yao bila kurejeshewa wanapostaafu,” anasema Katibu Mkuu huyo. Kuundwa kwa chama kipya hicho kumetajwa na wachambuzi wa mambo kwamba kunaweza kuipasua CWT na pia kutahitimisha ukiritimba wa muda mrefu mrefu wa chama hicho. Aidha, chama hicho kitatoa fursa sasa kwa walimu nchini kuwa na hiyari ya kujiunga na chama amb