SIWEMA ADAI MTOTO CURTIS SIO MTOTO WA NAY WA MITEGO, AMTAJA BABA YAKE.

Usiku huu kumezuka kutupiana maneno kati ya msanii wa Bongo Flava Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego na mama mtoto wake Siwema.

Kumezuka mjadala mkali kwenye mtandao wa Instagram mara baada ya Siwema kupost na kusema kwamba huyu mtoto wao Curtis sio wa Nay wa mitego na kutaja jina la Obasanjo kwamba ndiye baba halisi wa malaika huyu,na kuendelea kusema kwamba huyo  bwana ndiye alimvalisha pete.

Mashabiki wamezidi kuchafu hali zaidi na kuanza kumponda Siwema kwa kauli yake na wengine wenye busara kutoa ushauri swala hili lijadiliwe kifamilia na sio kwenye mitandao ya kijamii.

Ugomvi huu baina ya Siwema na Nay wa Mitego umeibuka hivi karibuni mara baada ya gazeti moja maarufu la udaku kuandika habari juu ya fumanizi alilolifanya Nay wa Mitego jijini Mwanza na kumkuta Siwema akiwa na Serengeti Boy, hali iliuompelekea Nay wa Mitego kumchukua mwanaye na kurudi naye jijini Dar Es Salaam.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA