Posts

Baraza la Maaskofu lazungumzia 'mgawo wa escrow' kwa Makasisi wake

Image
Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) limezungumzia sakata la maaskofu wa kanisa hilo, Methodius Kilaini na Eusebius Nzigirwa kudaiwa kupewa fedha za akaunti ya Tegeta Escrow na kusema kwa sasa hawawezi kuzungumzia suala hilo kutokana na kuwa linagusa watu binafsi. Limesema kuwa suala hilo halihusu baraza na inaweza kufanyiwa kazi kwa taratibu za kanisa kwa kadri uchunguzi unavyoendelea kufanyika, lakini sasa ni mapema mno. Msemaji wa Baraza hilo, Padri Anatoly Salawa alisema kwa sasa suala hilo wazungumzaji ni watu binafsi ambao wanahusika katika sakata hilo na siyo kama baraza. Alisema orodha inawahusu watu wengi na kwamba wakati mwafaka ukifika kanisa litatoa kauli, lakini suala hilo ni binafsi na askofu yeyote ana haki ya kufungua akaunti binafsi kama ilivyo kwa mtu yeyote. Alisema suala hapo linalohusu kanisa ni Benki ya Mkombozi, lakini hata hivyo benki haina mamlaka ya kumuuliza mteja alipopata fedha mpaka watilie shaka na kuto

LOWASSA AKANUSHA KUMILIKI AKAUNTI YA TWITA

Image
Toka bunge limeanza mjadala wa kadhia ya Escrow account,kuna mtu au kikundi kwa sababu wanazozijua wao wenyewe wameanzisha akaunti ya mtandao wa Twitter kwa jina la Edward Ngoyai Lowassa, @edwardlowasa. Kwa kutumia ukurasa huo, mtu huyo amekuwa akiandika masuala kadhaa kuhusiana na suala hilo la escrow account na kile kinachoendelea bungeni, ikionekana kama ni kauli ya Mh Lowassa. Tunawaomba wananchi  kupuuza yote yanayoandikwa katika ukurasa huo.Watanzania tuachane na tabia ya matumizi ya mitandao ya kijamii kupotosha umma,tutumie mitandao hiyo kwa kuhamasisha maendeleo,amani, umoja na mshikamano kwa taifa letu.   Imetolewa na ofisi ya Mh Edward Ngoyai Lowassa(Mbunge)

Andrew Nyerere; Mwalimu angekuwepo angepinga ufisadi!

Image
Kuna maswala kadha wa kadha yanayoikabili Tanzania kwa hivi sasa, miongoni mwa mambo haya ni sakata la akaunti ya Tegeta/Escrow, mchakato wa katiba mpya na mengine mengi. Mwandishi Nova Kambota amefanya mahojiano na Andrew Julius Nyerere ambaye ni mtoto wa kwanza wa baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere, fuatana naye katika mahojiano haya……………… SWALI; Kuna mambo kadhaa yaliyojitokeza siku za karibuni ambayo watu wanataka kufahamu manufaa yake kwa taifa, moja ya matukio hayo ni ziara ya Jafar Mermo  Idd Amin mtoto wa rais wa zamani wa Uganda marehemu Idd Amin mwaka 2008, je ziara hiyo ambayo ilimkutanisha na Madaraka Nyerere walipozuru Butiama ilikuwa na manufaa gani kwa taifa? JIBU; Kwa familia ya Mwalimu Nyerere na familia ya marehemu Idd Amin nadhani ilikuwa jambo zuri kuleta upatanishi, kuhusu kama taifa lilipata faida sijui. Aliongea Jafari kuhusu kuanzisha mfuko wa hela kuwasaidia wanajeshi walioathirika na vita vya Kagera(wa Uganda na Tanzania), pia nch

MAGAZETI YA LEO IJUMAA, NOVEMBER 28 YAPO HAPA

Image

Saratani ya tezi dume ni muuaji wa kimyakimya

Image
Watu wengi wamekuwa na shauku ya kutaka kujua ugonjwa wa saratani ya tezi dume, huku wakidhani ni mpya. Lakini ukweli ni kuwa umekuwapo miaka mingi na wengi wameugua. Takwimu zinaonyesha wanaume wengi huugua ugonjwa huu unaoongezeka kwa kasi ya hali ya juu. Kulingana na utafiti uliofanywa na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORIC), kutoka mwaka 2006, zinaonyesha kuwa kila mwaka kumekuwa na ongezeko la kesi mpya ya wagonjwa saratani ya tezi dume. Novemba ya kila mwaka, jumuiya za kimataifa huadhimisha tukio ambalo hujulikana kama Movemba. Maadhimisho hayo huhusisha kukuza kwa masharubu, kukusanya fedha na kuleta mwamko na ufahamu wa masuala ya afya kwa wanaume kama vile saratani ya tezi dume. Jina hilo la Movemba ni mchanganyiko wa neno ‘Masharubu na Novemba’. Maadhimi

Mikopo elimu ya juu yabagua masomo

Image
Dodoma. Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ritta Kabati ameihoji Serikali kuwa kwa nini Sera ya mikopo kwa elimu ya juu inatolewa kwa kozi za sayansi na ualimu badala ya kutoa mikopo kwa kozi zote. “Serikali hutenga fedha nyingi kila mwaka kwa ajili ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili vijana wanaojiunga na vyuo vikuu wakopeshwe, sasa kwa nini inaupendeleo?” alihoji. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenister Mhagama alisema utoaji wa mikopo hufuata taratibu za kisheria na miongozo ya Serikali hasa katika vipaumbele vya Taifa. “Mahitaji ya kitaifa ndiyo yanayoiongoza Serikali kuainisha programu zinazopewa kipaumbele katika kutoa mikopo kwa nia ya kuwashawishi wanafunzi wasome,” alisema. Alisema kuanzia mwaka wa masomo 2014/2015 vipaumbele vya Taifa ni Ualimu wa sayansi na Hisabati, Sayansi za Tiba, Uhand

BIRTHDAY PARTY YA RONA CHIZA YAFANA SANA

Image
Jana Alhamis ilikuwa ni siku ya kuzaliwa mke wa rafiki yangu Ramadhani Juma Kanzaga ambaye anaitwa Rona Chiza (Mama Akrama). Katika hali ya kumuacha katika mshangao yaani "suprise"mumewe aliamua kumfanyia sherehe yake ya kuzaliwa kwa kuwaarika marafiki zao wa karibu bila mkewe kufahamu katika hotel ya Tamal iliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar Es Salaam. Matukio katika picha.