Mikopo elimu ya juu yabagua masomo

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ritta Kabati ameihoji Serikali kuwa kwa nini Sera ya mikopo kwa elimu ya juu inatolewa kwa kozi za sayansi na ualimu badala ya kutoa mikopo kwa kozi zote.
“Serikali hutenga fedha nyingi kila mwaka kwa ajili ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili vijana wanaojiunga na vyuo vikuu wakopeshwe, sasa kwa nini inaupendeleo?” alihoji.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenister Mhagama alisema utoaji wa mikopo hufuata taratibu za kisheria na miongozo ya Serikali hasa katika vipaumbele vya Taifa.
“Mahitaji ya kitaifa ndiyo yanayoiongoza Serikali kuainisha programu zinazopewa kipaumbele katika kutoa mikopo kwa nia ya kuwashawishi wanafunzi wasome,” alisema.
Alisema kuanzia mwaka wa masomo 2014/2015 vipaumbele vya Taifa ni Ualimu wa sayansi na Hisabati, Sayansi za Tiba, Uhandisi wa umwagiliaji pamoja na gesi na mafuta.
“Sambamba na hilo, Serikali imeendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi wenye uhitaji wanaosoma kozi zisizo za kipaumbele na waliokidhi viwango vinavyotakiwa katika kupata mikopo,” alisema.
- Mwananchi

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA