Posts

PRECISION AIR YAONGEZA NDEGE MPYA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.Mohammed Babu akikata utepe kama ishara ya kuzindua ndege mpya ya Precision ART 42- 500 yenye uwezo wa kubeba abiria 48 ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es salaam na Bukoba na kurudi Dar es salaam, ndege hiyo iliruka kutoka Dar es salaam kwenda Zanziar na kurudi kwa majaribio na inatarajia kuanza safari zake mwezi ujao, wanaoshuhudia katika picha kutoka kulia ni Jamal Hussein Afisa Mtendaji Mkuu Citi Bank, Allan Sharra Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air na kushoto ni Rubani wa Ndege hiyo Chohan Mbarouk Mwana blog John Bukuku wa www.fullshangwe.blogspot.com akijiandaa kushuka mara baada ya ndege hiyo kurejea Dar es salaam ikitokea Zanzibar jana. Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye alikuwa mgeni rasmi Mh. Mohamed Babu katikati akisubiri ndege itue ili kufanya uzinduzi rasmi kwa kukata utepe kulia ni Allan Sharra Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air kushoto ni Jamal Hussein

KELV IN IN DA HOOD

Image
SIKU MOJA MOJA NA MIMI NIKIJIWEKA SIO MBAYA

MBAVU ZANGU MIE

Image
LEO Jumapili lazima tufurahi pamoja mpenzi wa blog hii ona mwenyewe kwa macho yako

Ravalomanana ahukumiwa kifungo

Image
Rais wa Madagascar anayeishi uhamishoni, amepewa hukumu ya kifungo cha maisha jela, na kazi ngumu kwa kutoa amri ya mauaji ya wafuasi wa upinzani. Marc Ravalomanana alihukumiwa bila ya yeye kuwepo mahakamani, kufuatia mauaji yaliyotokea mwezi Februari 2009, ya watu wasiopungua 30 na walinzi wake. Bw. ravalomanana amekuwa akiishi nchini Arika Kusini tangu mezi machi mwaka 2009. Watu waliouawa walikuwa wafuasi wa Andrey Rajoelina, ambaye hivi sasa ni rais. Bw. ravalomanana alishitakiwa kwa makosa ya mauaji na kuhusika katika mauaji, pamoja na washitakiwa wengine 18, wengine pia wakiwa wanaishi uhamishoni. Wakili mtetezi wa rais wa zamani, waliondoka mahakamani muda mfupi baada ya kesi kuanza kusikilizwa, wakisema mahakama hiyo inatumiwa na utawala wa Bw. Rajoelina "Lengo ni kumhukumu ili asiweze kurejea Madagascar na kushiriki katika uchaguzi siku zijazo," wak

Poulsen awatema Tegete, Yondani, wengine watano

KOCHA wa Taifa Stars, Jan Poulsen amewaacha wachezaji saba mahiri kwenye safari ya Algeria kwa sababu ambazo ameziita kuwa za kiufundi na ushindani mkubwa kwenye kikosi chake. Kikosi hicho cha wachezaji 20 kitakachoondoka Jumanne kwenda Algeria kwa mchezo huo wa kwanza za kusaka tiketi ya kufuzu kwa fainali za Afrika mwaka 2012. Timu hiyo itaondoka kwa ndege ya Shirikika la Ndege la Qatar Airways kuelekea Algiers. Wachezaji walioachwa ni pamoja na Uhuru Seleman, Kelvin Yondani, Juma Jabu, Abdulhalim Humoud , Jerryson Tegete, Athuman Idd 'Chuji' na kipa Juma Kaseja. Poulsen alisema wachezaji hao wameachwa kwa sababu mbalimbali za kiufundi. Alisema Chuji na Kaseja bado ni majeruhi. “Chuji amepata nafuu , lakini hajakuwa na mazoezi kwa muda mrefu, siwezi kusafiri naye kwani hawezi kucheza, hali ambayo ni sawa kwa Kaseja ambaye nimempa muda zaidi wa kupona,” alisema Poulsen. Aliongeza kuwa Abdulhalim Humud, ambaye anaichezea Simba ameachwa kwa sababu ya timu yake kuwa na viungo wan

HAPPY BIRTHDAY JOH MAKINI

Image
Leo ni birthday ya Mwamba wa kaskazini kutoka Atown city,wish all da best katika Game also katika maisha yako we celebrate together

MAKAMUZI YANAELEKEA SEATTLE 28-AUG BAADA YA KASAS CITY

Image
Haya kazi kwenu wana wa EAST AFRICA mnaoishi mitaa ya SEATTLE,mwana HAULE yupo kwenu tayari kukinukisha mbaya vilivyo…show itafanyika tarehe 28 AUGUST katika ukumbi wa AFRIQ LOUNGE...usikose baab

BBA ALL STARS KURUKA BONGO FLEVA WIKI HII..

Image
Jmosi wiki hii..Dj Stive B kutoka Clouds fm atachapa ngoma kali za ukweli hasa Bongo flevaz ndani ya mjengo wa BBA All Stars na kuwarusha washiriki wote mjengoni...huu ni utaratibu mpya wa BBA All Stars mwaka huu kuwafurahisha washiriki na kuwafanya wa-enjoy weekend kila j'mosi kwa kuwaalika ma-djs mbalimbali toka nchi mbalimbali za Afrika kupiga ngoma mjengoni pale...safari hii ni zamu ya Bongo na Dj aliyebahatika kupata zali hilo ni Stive B aka Skillz...kazi kwenu fans kufuatilia nini kitajili siku hiyo

KATIZA ANGA YAO UONE SHUGHULI

Image
Ni askari wa kikosi cha kuzuia na kutuliza fujo Tanzania, Field Force Unit, (FFU) al maaruf Fanya Fujo Uone, wakiwa katika mavazi yao rasmi tayari kwa kukabiliana na purukushani zozote ambazo zinaweza kuchomoza kutokana na kutokukubaliana katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Wabunge na Raisi.

TAHADHARI KWA WAPENDA KULA KARANGA JIANI

Image
Mfanyabiashara ndogondogo wa karanga ambaye jina lake halikujikana akiokota karanga zilizomwagika jana nje ya Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam (? na kuzichanganya kwenye zilizomo kwenye kifuko cha biashara?). Hatua hiyo inahatarisha afya za walaji kwa kuwa upo uwezekano wa kijana huyo kuziuza tena kwa wateja wake bila wao kujua kama sio salama. Mtizamaji, tizama mwelekeo wa mikono hiyo unaookota karanga, hizo zinaelekea kutupwa au kuchanganywa'mo? Ikiwa alikuwa na nia ya kuzitupa, kwa kawaida huwa tunafyagia kwa mguu kuelekea pembeni ikiwa mikono tayari imebeba kitu, ama, kile kilichobebwa huwekwa mbali na mwelekeo wa mikono au miguu huwa upande wa ardhini (kama ni kutoka kwenye sakafu) au huwa tunaacha na kusonga mbele. Matatizo ya kiafya ya magonjwa ya mlipuko vyanzo vyake ni vya aina hii kwani sehemu kinapookotwa chakula huwa imekanyagwa na viatu vilivyopita maeneo machafu sana ikiwemo vyooni na majalalani.

JAY-Z AND BEYONCE ENJOYING IN ITALY

Image
Jay-Z and his wife Beyonce are currently enjoying a romantic vacation in Italy. The couple were spotted strolling the streets of Portoferraio last Friday.

NAFAZI ZA KAZI MBALIMBALI

MANAGER TECHNICAL SERVICES SECTION Qualification: Holder of BSc. Engineering in Electronics and Telecommunications Apply: The Director General, Tanzania Meteorological Agency Box 3056, Dar es Salaam Details: Mwananchi, August 16, 2010. Deadline: September 02, 2010 HEAD LEGAL OFFICER Qualification: Holder of Bachelors of Law (LLB) Apply: The Director General, Tanzania Meteorological Agency Box 3056, Dar es Salaam Details: Mwananchi, August 16, 2010. Deadline: September 02, 2010 ENGINEER Qualification: Holder of degree in Engineering or Advanced diploma in Engineering (Telecommunications/Electronics) Apply: The Director General, Tanzania Meteorological Agency Box 3056, Dar es Salaam Details: Mwananchi, August 16, 2010. Deadline: September 02, 2010 REGISTRY CLERK Qualification: Holder of Advanced certificate of Secondary Education with passess in English Apply: The Director General, Tanzania Meteorological Agency Box 3056, Dar es Salaam Details: Mwananchi, August 16, 2010. Deadline: Septe