TAHADHARI KWA WAPENDA KULA KARANGA JIANI


Mfanyabiashara ndogondogo wa karanga ambaye jina lake halikujikana akiokota karanga zilizomwagika jana nje ya Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam (? na kuzichanganya kwenye zilizomo kwenye kifuko cha biashara?). Hatua hiyo inahatarisha afya za walaji kwa kuwa upo uwezekano wa kijana huyo kuziuza tena kwa wateja wake bila wao kujua kama sio salama.

Mtizamaji, tizama mwelekeo wa mikono hiyo unaookota karanga, hizo zinaelekea kutupwa au kuchanganywa'mo? Ikiwa alikuwa na nia ya kuzitupa, kwa kawaida huwa tunafyagia kwa mguu kuelekea pembeni ikiwa mikono tayari imebeba kitu, ama, kile kilichobebwa huwekwa mbali na mwelekeo wa mikono au miguu huwa upande wa ardhini (kama ni kutoka kwenye sakafu) au huwa tunaacha na kusonga mbele.

Matatizo ya kiafya ya magonjwa ya mlipuko vyanzo vyake ni vya aina hii kwani sehemu kinapookotwa chakula huwa imekanyagwa na viatu vilivyopita maeneo machafu sana ikiwemo vyooni na majalalani.


Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA