Posts

Picha: Maziko ya Whitney Houston

Image
Gari iliyobeba maiti ikielekea kanisani Waombolezaji wakifika kanisani Kitabu cha maombolezo kikiwa kinajaa saini za waombolezaji Jeneza ikitolewa kanisani na kupelekwa kwenye sehemu ya kuzikia Ray J (aliyezungushiwa duara jekundu) akiligusa jeneza la aliyekuwa mpenzi wake Whitney Houston Ulinzi ulikuwepo wa kutosha Bobby Brown (mwenye miwani) akihudhuria mazikoni, lakini alizuiliwa kuingiaa na wageni wake ambao walikuwa tisa. Yeye alipewa mualiko wa mpaka wageni wawili tu. Bobby Brown akiondoka msibani hapo baada ya kukataliwa kuingia kanisani na wageni wake wote aliokwenda nao Kevin Costner akitoa nasaha zake msibani hapo Steve Wonder akiimba msibani hapo Tyler Perry nae alikuwa na machache ya kusema Alicia Keys akiimba Wana kwaya wakiimba msibani hapo katika kanisa ambalo ndilo Whitney alipoanzia kuimba

WALIMU WAPYA WAANDAMANA RORYA

ZAIDI ya walimu wapya   40 wameandana na kulala katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya Rorya zilizoko Ingiri juu kushinikiza kulipwa pesa yote ya kujikimu ya siku saba. Hali hiyo imekuja baada ya walimu hao kubaini kuwa katika Wilaya zingine wenzao walilipwa kiasi tofauti na wao. Wakizungumza na waandishi wa habari mapema asubuhi jana walimu hao walieleza kuwa kulipwa pesa ya siku nne kunawafanya washindwe kuandaa maisha yao mapya vizuri na pesa hiyo haitatoshi kulingana na mazingira yalivyo Wilayani humo. “Tuliamua kutembea kwa miguu na kuja kulala hapa ili uongozi uone kuwa hatukubaliani ha kiasi hicho cha pesa ya kujikimu wanachokitoa kwetu” alisema mmjoja wa walimu hao ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini. Walisema kuwa kati ya walimu 160 walioajiriwa katika Halimashauri hiyo wakiwemo walimu wachache wa shule za sekondari, baadhi yao walipokea kiasi cha shilingi 140,000 ambacho ni cha siku nne na waliobaki walikataa wakidai wa

Hiki ni kizazi cha TEKNOHAMA

Image
 

SSPRA WAFANYA ZIARA KATIKA KAMPUNI YA NYANZA BOTTLING

Image
Wanafunzi wa chuo cha mtakatifu Augustino (Mwanza )wanaosoma shahada ya Uhusiano wa Umma na Masoko ,leo wamefanya ziara ya mafunzo katika kampuni ya Cocacola (Nyanza Bottling Company Limited).Ili kupata mafunzo mbalimbali kuhusiana namna uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo unavyofanyika. Ziara hiyo iliandaliwa na chama cha wanafunzi wasomao uhusiano wa Umma SSPRA (SAUT STUDENT’S PUBLIC RELATIONS ASSOCIATION)iliandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya vitendo kwa wanachama wao hususani katika uhusiano wa umma na masoko yanayofanya na kampuni hiyo. Aidha wakati wa mafunzo hayo maswali kadhaa yaliulizwa hasa pale wanafunzi walipotaka kujua wapi malighafi zinatolewa kwaajili ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo,kufuatia swali hilo mwelimishaji alibainisha kuwa malighafi nyingi zitumikazo katika uzalishaji kama vile sukari ,uzalishaji wa chupa hutoka chi za nje kama vile Brazil, Saudi Arabia, Afrika kusini sababu zilizotolewa na mwe