WALIMU WAPYA WAANDAMANA RORYA
ZAIDI ya walimu wapya 40
wameandana na kulala katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya Rorya
zilizoko Ingiri juu kushinikiza kulipwa pesa yote ya kujikimu ya siku
saba.
Hali hiyo imekuja baada ya walimu hao kubaini kuwa katika Wilaya zingine wenzao walilipwa kiasi tofauti na wao.
Wakizungumza
na waandishi wa habari mapema asubuhi jana walimu hao walieleza kuwa
kulipwa pesa ya siku nne kunawafanya washindwe kuandaa maisha yao mapya
vizuri na pesa hiyo haitatoshi kulingana na mazingira yalivyo Wilayani
humo.
“Tuliamua
kutembea kwa miguu na kuja kulala hapa ili uongozi uone kuwa
hatukubaliani ha kiasi hicho cha pesa ya kujikimu wanachokitoa kwetu”
alisema mmjoja wa walimu hao ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini.
Walisema
kuwa kati ya walimu 160 walioajiriwa katika Halimashauri hiyo wakiwemo
walimu wachache wa shule za sekondari, baadhi yao walipokea kiasi cha
shilingi 140,000 ambacho ni cha siku nne na waliobaki walikataa wakidai
walipwe pesa yote ya siku saba.
“Mimi nina mke na sina chombo cha ndani hata kimoja wakinipa shilingi 140,000/- kitanisaidia nini na bei ya vitu iko juu nitaishije sina kitu ndani? Alihoji Mwalimu Musa Abdi.
Kutokana
na maandamano hayo uongozi wote wa Wilaya hiyo ulifanya kikao na walimu
hao na kuwaomba wapokee kiasi hicho ambachokipo na watalipwa kwa kuwa
hakuna pesa ya kutosha katika halmashauri hiyo.
Afisa
elimu wa Wilaya hiyo Michael Igogo alisema kuwa wanafanya mazungumzo na
RAS na TAMISEMI kuona namna ya kutatua tatizo hilo linalowakabili, na
kuongeza kuwa hoja yao ni ya msingi.
“Hoja
zao ni kuwa kwa nini hawalipwi pesa zote kama Wilaya zingine, lakini
Wilaya hizo zina mapato makubwa.Hata hivyo tumeamua kuwalipa sawa wote
shilingi 245,000/-“ alisema Igogo.
Ofisa
huyo aliongeza kuwa kati ya walimu waliopangiwa Wilayani humo wengine
walipelekewa pesa zao vituoni mwao ili kuondoa usumbufu wa wao
kufuatilia pesa hizo ofisini badala ya kuwahudumia wanafunzi.
“Hawa
ni wale waliochelewa kuripoti na kutokana na kuwa hatuna pesa za
kutosha tumeamua kuwapa kiasi hicho cha siku nne halfu tutawamalizia
kiasi cha siku tatu baada ya kurekebisha mambo” alisema afisa Elimu
huyo.
Comments
Post a Comment