SSPRA WAFANYA ZIARA KATIKA KAMPUNI YA NYANZA BOTTLING
Wanafunzi
wa chuo cha mtakatifu Augustino (Mwanza )wanaosoma shahada ya Uhusiano
wa Umma na Masoko ,leo wamefanya ziara ya mafunzo katika kampuni ya
Cocacola (Nyanza Bottling Company Limited).Ili kupata mafunzo mbalimbali
kuhusiana namna uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo
unavyofanyika.
Ziara hiyo iliandaliwa na chama cha wanafunzi wasomao uhusiano wa Umma SSPRA (SAUT STUDENT’S PUBLIC RELATIONS ASSOCIATION)iliandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya vitendo kwa wanachama wao hususani katika uhusiano wa umma na masoko yanayofanya na kampuni hiyo.
Aidha
wakati wa mafunzo hayo maswali kadhaa yaliulizwa hasa pale wanafunzi
walipotaka kujua wapi malighafi zinatolewa kwaajili ya uzalishaji wa
bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo,kufuatia swali hilo mwelimishaji
alibainisha kuwa malighafi nyingi zitumikazo katika uzalishaji kama vile
sukari ,uzalishaji wa chupa hutoka chi za nje kama vile Brazil, Saudi
Arabia, Afrika kusini sababu zilizotolewa na mwelimishaji bwana Mlekwa Pius aliyoko Sugar Store kuhisiana na uagizaji wa sukari kutoka nchi za nje alisema kuwa makampuni
yanayohusika na uzalishaji wa sukari hayakidhi viwango vinavyohitajika
kwa ajili ya uzalishaji wa soda hivyo inasababisha serikali kukosa
mapato.
Uongozi
wa SSPRA unapenda kutoa shukrani zake kwa Uongozi wa Kampuni ya Nyanza
Bottling kwa kuweza kufanikisha ziara yao na kwa wafanyakazi wao ambao
wameweza kutoa mafunzo kwa wanachama wa SSPRA bila kuchoka pale
walipokuwa wanaulizwa maswali.
Mashine inayotumika kutengenezea chupa za plastic za soda
chupa zinapita kwenye mitambo kwa ajili ya kusafishwa
ndani ya chumba cha usafishaji chupa
baada ya kuangalia uzalishaji wa chupa wanachama wakachukua japo picha ya ukumbusho.
Anthonius pamoja na Francis wakishangaa hatua ya kwanza ya chupa ya plastic kabla haijaingizwa kwenye mashine kujazwa upepo
Hizi ndo chupa za plastic kabla hazijawekwa kwenye
mashine kwa hatua ya mwisho kuwekewa upepo iweze kupanuka kwa ajili ya
kuwekewa soda
Ndani ya chumba cha utengenezaji wa maumbo mbalimbali ya chupaMembers wakiwa nje wakisubili kuingia ndani.
Anajulikana kwa jina la bwana Dotto Andrew
ambaye yuko stoo ya sukari,alikuwa anatoa maelezo mbalimbali juu ya
uchanganyaji wa sukari na kiwango kinachohitajika kwa kila soda
Nyanja and Ally
Nyanja and Daniel
Anthonius and Daniel
Mwenyekiti wa SSPRA upendo Kessy akiwa na Francis Moses mwenyekiti wa kamati ya Uhusiano wa vyombo vya habari na machapisho
Nyanja and Zawadi
Jacqueline Patrick Katibu msaidizi wa SSPRA
Erick Charles na Magafu
Comments
Post a Comment