Posts

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 24/12/2012 HAYA HAPA

Image
. . . . . . .

Ujumbe wa Christmas wa Papa Benedict

Image
Kiongozi wa waumini wa kikatoliki duniani Papa Benect XVI ameitumia nafasi ya kutoa ujumbe wa Christmas kushambulia ndoa za jinsia moja, na kuwatuhumu mashoga kuwa ni watu ambao wanaubadilisha uhalisia wao ili waweze kuendana na jinsia ambayo ni chaguo lao. Papa Benedict ame-dedicate hotuba yake kwa “thamani ya familia na ubora wa familia”, na alisema kuwa umoja wa desturi nzuri umeshambuliwa na sheria ya ndoa za jinsia moja ikipata sapoti Uingereza, Marekani na Ufaransa. Alisistiza kuwa theories za jinsia hazikua sahihi, na kuongeza kuwa watu walikuwa wamepotoka kwa kuchagua utambulisho wao kijinsia kitu ambacho kilikuwa kinyume na uhalisia. Hapa Papa Benect alikuwa anapinga theories ambazo ziliibuka miaka 85 iliyopita baada ya kuanzishwa na Simone de Beauvoir, na kuitwa Beauvoir’s gender theory toka kwa mwanafalsafa aliyekuwa mwanaharakati wa kupigania haki za wanawake, theory ambayo ilikuwa inasema, “mwanamke hazaliwi mwanamke bali ‘anakua’ mw

WANACHAMA WA SSPRA WATOA MSAADA KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA,JIJINI MWANZA

Image
Wanachama wa SSPRA leo tarehe 15/12/2012 wametembelea na kutoa misaada ya chakula na malazi kwa ajili ya kuwasaidia watoto walioko kituo cha STAREHE CHILDREN'S HOME kilichopo eneo la Nyegezi jijini Mwanza, wanachama wa SSPRA wametoa msaada huo kwa watoto yatima katika kuelekea sherehe za mwisho wa mwaka  X-MASS na mwaka mpya ikiwa ni mojawapo ya majukumu ya kuisaidia jamii inayotuzunguka (CORPORATE SOCIAL RESPONSIBILITY). Kituo hiki kinahudumia watoto yatima,waliotelekezwa kuanzia umri wa miaka 0-5, watoto hawa huletwa kituoni hapo kutoka Ustawi wa jamii na sio kwamba wao ndio huwatafuta watoto hao. BW.GETSON EZEKIEL ambaye ni Daktari wa watoto hao walioko kituoni hapo. Baadhi ya watoto walioko kituoni hapo wakipokea msaada kutoka SSPRA Joseph Michael akimkabidhi Dr. Ezekiel  kadi ya X-MASS na Mwaka Mpya. Watoto waliopo kituoni hapo wa Muddy akikabidhi naye zawadi yake kwa mtoto wanachama wakifika kituoni hapo muda wa asubuhi.

VICHWA VYA MAGAZETI LEO ALHAMIS,DEC 13

Image
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Mandela atibiwa ugonjwa wa mapafu

Image
Chapis Mzee Nelson Mandela Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela amepatwa tena na ugonjwa wa mapafu na anaendelea vyema na matibabu . Bwana Mandela ambaye ana umri wa miaka 94, amekuwa hospitalini mjini Pretoria tangu Jumamosi . Taarifa zinazohusiana Afrika Kusini Hii ni taarifa ya uhakika ya kwanza kutolewa kuhusu afya ya kiongozi huyo aliyepinga utawala ubaguzi wa rangi . Bw mandela alitibiwa mapafu miaka 2 iliyopita. Habari kuwa Mandelela anatibiwa ugonjwa wa mapafu, bila shaka imemaliza wasiwasi wa siku kadhaa kuhusu ukosefu wa taarifa zozote kuhusu afya yake Wananchi wa Afrika Kusini wanafuatilia kwa maakini taarifa za afya ya Mandela Msemaji wa rais huyo mstaafu hakueleza kuhusu ikiwa hali ya Mandela ni mbaya sana au itakuwa sawa lakini alisisitiza kuwa anaendelea kupokea matibabu. Miaka miwili iliyopita, hali kama hii ilijitokeza kuhusu Mandela baada ya kulazwa hospitalini kwa tatizo la kupum

Nguo fupi alias ‘vimini’ ni marufuku Vyuo vya KKKT

Habari imeandikwa na Yusuph Mussa -  Majira , Lushoto, Tanga MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kilichopo jijini Arusha, Profesa Joseph Parsalaw, amesema kuqanzia sasa ni marukufu kwa wanawake wanaosoma katika vyuo vikuu vyote na vile vishiriki vinavyomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), kuvaa suruali za kubana au vimini. Prof. Parsalaw aliyasema hayo juzi katika mahafali ya tatu ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU), kilichopo Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga na kusisitiza kuwa, lengo ni kutoa wahitimu ambao watakubalika kwenye jamii kwa matendo yao pamoja na uvaaji wao. “Chuo Kikuu cha Tumaini kipo mstari wa mbele kuwahimiza wanafunzi na wafanyakazi kuzingatia maadili  anayokubalika kwenye jamii ya Kitanzania.  Hivi sasa katika vyuo vyote vishiriki, tumeweka bayana aina ya mavazi ambayo yanastahili kuvaliwa na vijana ili kudumisha heshima na maadili mema,” alisema Prof. Parsalaw. Naye Makamu Mkuu wa Chuo cha SEKOMU, Mchungaji Dkt