KUTOKA KATIKA FACEBOOK WALL YA ALIYEKUWA RAIS WA CHUO CHA SAUT Malisa Godlisten AFUNGUKA Kwanza kabisa, natoa pole za dhati kwa familia, ndugu jamaa, marafiki na jumuia yote ya chuo cha uhasibu Arusha (IAA) kwa kifo cha mwanafunzi Henry Kago aliyefariki juzi usiku kwenye tukio la kutisha na kuhuzunisha, kwa kuchomwa visu shingoni. Mungu awapatie faraja na utulivu katika kipindi hiki kigumu. Lakini kuna mambo lazima tuyaseme kama tuna nia ya kujali maisha ya wanafunzi waliopo vyuo vya elimu ya juu. Kwanza hali ya usalama ktk vyuo vingi ni mbovu sana. Matukio ya kuvamiwa, kubakwa, kuteswa, kuporwa na hata kuuawa kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu imekuwa jambo la kawaida, na yanaripotiwa kila siku. Lakini serikali haichukui hatua as if mambo hayo yanatokea Dubai. Serikali imeshindwa kutoa msaada wowote badala yake wanakuwa mstari wa mbele kuattack wanafunzi wanapodai haki yao ya ulinzi. Pale chuo cha St.John aliuawa mwanafunzi mmoja akiwa ametoka chuoni k