PICHA ZA WASANII WALIOSHIRIKI KATIKA KUFANYA USAFI KATIKA MAKUBURI YA MV.BUKOBA JIJINI MWANZA HIZI HAPA





















NA ALBERT G. SENGO:
Wasanii wa muziki wa Nyumbani (Bongo Fleva) Kala Jeremiah, H. Baba, Kitale na mwanadada Dyna leo wameshiriki zoezi la kusafisha mazingira ya makaburi ya watu waliofariki dunia kwenye ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Bukoba, makaburi yaliyoko Igoma nje kidogo ya jiji la Mwanza.

Zoezi hilo limekuja mara baada ya mmoja kati ya wasanii hao (H. Baba) kupita katika eneo hilo na kujionea hali mbaya ya mazingira ndipo alipochukuwa jukumu la kuwasilisha taarifa hiyo kwa wasanii wenzake ambapo uungwaji mkono ulikuwa wa asilimia mia moja.

Mapema leo shughuli za usafi zilianza kushika kasi, zoezi ambalo liliwachukuwa takribani masaa manne kumalizika likuwa gumu kutokana na magugu na nyasi nyingi kumea kwenye eneo hilo la makaburi kiasi cha kuwasababisha wasanii hao kuongeza zana zaidi za usafi ili kuweza kufikia lengo lao

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA