Malisa Godlisten AFUNGUKA JUU YA MAUAJI YA HENRY KAGO WA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA, SERIKALI IWAJIBIKE.!



Kwanza kabisa, natoa
pole za dhati kwa familia, ndugu
jamaa, marafiki na jumuia yote ya chuo cha uhasibu Arusha (IAA) kwa kifo cha mwanafunzi Henry Kago aliyefariki
juzi usiku kwenye tukio la kutisha na kuhuzunisha, kwa kuchomwa visu shingoni. Mungu awapatie faraja na utulivu katika
kipindi hiki kigumu.

Lakini kuna mambo lazima tuyaseme kama tuna nia ya kujali maisha ya wanafunzi waliopo vyuo vya elimu ya juu.

Kwanza hali ya usalama ktk vyuo vingi ni mbovu sana. Matukio ya kuvamiwa, kubakwa, kuteswa, kuporwa na hata kuuawa kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu imekuwa jambo la kawaida, na yanaripotiwa kila siku.

Lakini serikali haichukui hatua as if mambo hayo yanatokea Dubai. Serikali imeshindwa kutoa msaada wowote badala yake wanakuwa mstari wa mbele kuattack wanafunzi wanapodai haki yao ya ulinzi.

Pale chuo cha St.John aliuawa mwanafunzi mmoja akiwa ametoka chuoni kujisomea usiku. Kwanza alibakwa kisha akauawa kikatili. Serikali haikuchukua hatua yoyote kuwasaka wahalifu. Hakuna Polisi yeyote aliyefika eneo la tukio. Wanafunzi wakaona serikali haina msaada, wakaamua kuandamana kumlilia mwenzao. Kuona maandamano Polisi wakamiminika chuoni kama nzige.

Polisi wakapambana na wanafunzi walioandamana badala ya kupambana na majambazi waliomuua mwanafunzi. Wakawapiga mabomu ya machozi na virungu. Eti wanavuruga amani. Hivi kati ya wale wauaji waliobaka na kuua, na hawa wanafunzi wanaoandamana kudai haki yao ya kulindwa, nani anavuruga amani??

Tukio la mauaji ya Henry kule IAA linafanana kbs na tukio la St.John. Ndugu yetu huyu alitoka library usiku anakwenda hostel. Kutokana na mfumo mbovu wa usalama, akavamiwa na majambazi ambao licha ya kumpora walimchoma visu shingoni, na kusababisha majeraha yaliyopelekea kifo chake. Mwenzie aliyejitokeza kumsaidia akachomwa kisu tumboni.

Jeshi la Polisi walipewa taarifa lakini hawakuchukua hatua zozote kuwatafuta wahalifu.

Mkuu wa Mkoa akapewa taarifa lakini hakwenda hata kutoa pole. That means alipuuza.

Mbunge wa Arusha Mjini Mh.Lema akapata taarifa akafika eneo la tukio kuwapa pole na kuwatuliza wanafunzi waliokuwa na uchungu wa kumpoteza mwenzao. Hadi hapa mi nadhani Lema alistahili kupongezwa kwa kuonesha concern kama mbunge wa eneo husika.

RC Magesa kusikia Lema yuko chuoni nae akaenda. Si kuonesha concern ya kifo cha Henry, bt kutafuta credit over Lema.

Wanafunzi kumuona wakamzomea coz mwanzoni hakuonesha umuhimu wa kwenda hadi aliposikia Lema ameenda. So they had to pay more attention kwa Lema aliyekuja kuwasiliza than RC Magesa aliyekuwa kum win Lema. Hawakuwa na time nae, hawakumsikiliza, wakamzomea. Lema akawa anajitahidi kuwatuliza ili wamsikilize RC lakini RC tayari alikuwa kashawakera.

RC kuona hivyo akakasirika na kuagiza Lema akamatwe. Liko wapi kosa la Lema? Kwenda chuoni wakati chuo kipo jimboni kwake? Kujaribu kuwatuliza wanafunzi na kuwafariji? Kusikilizwa zaidi kuliko RC or what?

Na katika kuonesha kuwa serikali haijali kifo cha Henry, saivi hoja iliyopo ni Lema kufanya vurugu badala ya kudiscuss namna ya kuwakamata wahalifu waliofanya mauaji. That means maadui wa Polisi sio wale Majambazi waliofanya mauaji, adui wa polisi ni Lema. Huu ni wendawazimu.

Henry amekufa bila msaada wowote wa askari polisi. Hakuna polisi yeyote aliyekuwa karibu wakati Henry anajaribu kuokoa roho yake. Eti kuna uhaba wa polisi mkoani Arusha wa kufanya patrol. Lakini waliposikia maandamano walitokea polisi wasio na idadi. Polisi wakakaribia kuzidi idadi ya anafunzi pale chuoni. Sijui walitoka wapi, wakati Arusha kuna uhaba wa polisi.

This means Polisi wanatumia nguvu kubwa kupambana na maandamano, kuliko nguvu wanayoitumia kupambana na wahalifu waliofanya mauaji. Nina wasiwasi hakuna Polisi yeyote anayefanya upelelezi wa kuwatafuta hao wauaji, maana wote wako busy kumtafuta Lema. Huu ni upuuzi.!

Mwaka jana mwezi October nilipokutana na Waziri Mulugo nilimweleza changamoto ya ulinzi ktk vyuo vingi nchini. Watu wanatekwa, wanavamiwa, wanabakwa, wanaporwa na hata kuuawa. Serikali ina mkakati gani wa kukomesha hali hii? Jeshi la polisi liko wapi? Au linasubiri watu wauawe then lianze kupambana na watakaoandamana. We should be proactive than reactive.

Ni ajabu mtu akiuawa polisi hawafanyi lolote, lakini ukihoji kwnn fulani kauawa unaonekana mhalifu. Unaambiwa unachochea mgomo au maandamano. Huu ni upuuzi wa kiwango cha juu. Na jeshi la Polisi la Tanzania ndio jeshi pekee linaloweza kufanya upuuzi kama huu dunia nzima.

Kuna haja ya kufanya mabadiliko ya kimfumo ktk jeshi letu la polisi. Kauli mbiu ya Jeshi la polisi ni usalama wa raia. Lakini kwa yanayotokea ni kama vile kauli mbiu ni "Usalama wa wahalifu na mateso kwa Raia"

Nchini Zambia, Polisi kwao si jeshi, ni huduma kama zilivyo huduma nyingine za jamii. Ndio maana wao wanaita "Zambia Police Service" kwetu tunaita "Tanzania Police Force"

Kuna haja ya polisi wetu kuwa "service" badala ya "force"
Polisi iwe huduma kama zilivyo huduma za maji na elimu. Na kwa kuwa huduma za jamii ni lazima, hivyo Polisi ikiwa "service" suala la usalama wa raia na mali zao litakuwa suala la lazima pia.

Bt tukiendelea kubaki na hii "force" tutaendelea kulinda wahalifu wanaoua wasomi wetu, na kukimbizana na akina Lema kisa ameshangiliwa zaidi ya mkuu wa mkoa. Upuuzi!!!

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA