Posts

MARCOS ROJO ATIMKIA MANCHESTER UNITED

Image
Marcos Rojo amewasili England kwa ajili ya kukamilisha usajili wake Manchester United. KLABU ya Manchester United imekubali kutoa Pauni Milioni 16 kumnunua beki wa Sporting Lisbon, Marcos Rojo. Rojo, ambaye ametua mjini Manchester na kusema kuhamia United 'anahisi kama ndoto', anatarajiwa kusaini Mkataba wa miaka minne akifaulu vipimo vya afya na kukubali vipengele binafsi vya kandarasi yake. Louis van Gaal ametoa kipaumbele kwa usajili wa beki huyo mtumia mguu wa kushoto, Rojo, mwenye umri wa miaka 24, kufuatia kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England Jumamois na Swansea. Winga Luis Nani, aliyejiunga na United kutoka Sporting kwa Pauni Milioni 17 mwaka 2007, amerejeshwa kwa mkopo klabu yake hiyo ya zamani, ilia ni sehemu ya dili hilo la Rojo.

VIDEO MPYA YA NICKI MINAJ "ANACONDA" YAFIKISHA WATAZAMAJI 5,856,035 KABLA YA SIKU KUISHA

Image
Video ya music inayoendelea kushikilia record kutoka youtube ni ya PSY ya "Gangnam style" ambayo mpaka sasa ina zaidi ya watazamaji 2,066,230,670 tangu ilipotoka December 21,2012 . Video hii mpya ya Nicki Minaj " Anaconda" uwenda ikavunja record hiyo, video hii imekuwa gumzo kote duniani hasa kwa wapenzi wa muziki, Je ni nini haswa kimefanya video hii iweze kutazamwa zaidi na kufikisha watazamaji 5,856,035 mara baada ya kuwekwa ikiwa haijamaliza hata siku moja tangu kuwekwa kwake kwenye account yake ya vevo ya youtube?. Lugha iliyotumika sio nzuri kabisa lakini utata mkubwa uko katika mavazi yaliyotumika kwa upande wa akina dada wanaoonekana katika video hii na Nicki Minaj mwenyewe alivyo vaa na kutingisha booty.

PICHA KALI NNE ZA UTATA KATI YA NICKI MINAJ NA RAPPER DRAKE KUTOKA KATIKA VIDEO YA "ANACONDA"

Image
Nicki Minaj kupitia account yake ya instagram  amepost baadhi ya picha zilizochukuliwa katika utengenezaji wa video yake ya Anaconda inayotarajiwa kuachiwa kesho Jumatano 20/8/2014 kupitia account yake ya VEVO ya Youtube.  Rapper Drake ameonekana kwenye video hii iliyotayarishwa na Colin Tilley. Nicki Minaj atafanya show ya Mtv Video Music Awards na huu wimbo wake mpya kutoka kwenye album ya The Pink Print.

VIDEO: TIZAMA VIDEO TEASER YA NEY WA MITEGO -"MR. NAY"

CHELSEA YAANZA LIGI KUU KWA KUICHAPA BURNLEY

Image
  Tembo: Didier Drogba akipiga shuti kujaribu kufunga goli baada ya kuingia katika dakika za lala salama  MBWATUKAJI Jose Mourinho ameanza ligi kuu England ‘Swafii’ kabisa baada ya kufanikiwa kuingoza ugenini Chelsea kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu mpya ya Burnley. Wenyeji ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 15 kupitia kwa Scott Arfield,  lakini mshambuliaji mpya wa Chelsea, Diego Costa alifungua akaunti ya mabao katika mechi za ligi kuu baada ya kuifungia timu yake bao la kusawazisha katika dakika ya 17. Akaunti ya magoli: Diego Costa akifunga bao lake la kwanza la ligi kuu  Wakati Burnley wakiwa na matumaini ya kuongeza bao, Mjerumani, Andre Schurrle aliifungia Chelsea bao la kuongoza katika dakika 21 na Branislav Ivanovic akahitimisha karamu ya mabao katika dakika ya 34. Tatizo kubwa kwa Burnley ni kwamba wachezaji wake hawajawahi kukutana na kitu kama hiki, hivyo kujikuta wakizidiwa maarifa kimbinu

MAGAZETI YA LEO JUMANNE, AUGUST 19 YAPO HAPA.

Image

LULU AONYESHA MSISITIZO WAKE WA KUMPENDA MWANAMZIKI JUSTIN BIEBER

Image
Elizaberth Michael maarufu kama Lulu ameendelea kushikilia msimamo wake wa kumpenda mwanamziki Justine Bieber   officiallulumichael Mapemaaaa...Kabla cku haijawa ngumu..! Haya ni hv wale wa kuandika ndoto za nn cjui...Mara cjui huwezi kumpata na cjui kimepanda kimeshuka...msinijazie comment😂😂😂Acha niwape ufafanuzi kdgo...ni hv Huyu Bwana swala ya yy kupenda....nimemwachia awapende kina @selenagomez na wengine wote anaotaka kuwapenda...ila swala la yy kupendwa Aniachie Mimi....yan hyo kazi yangu....!!!Sasa Kama ni ndoto Wallah ctaki kuamka,Kama ni ufala...yani ninaukubali kwa asilimia 150%,na mengine mengine yote...sasa Kama nakuchefua,Nina uhakika Zile ndimu za @diamondplatnumz haziwezi kukutosha mana hiki kichefuchefu co cha kuisha,bora utafute mbegu ya Malimao au mbilimbi upande kwako kbsa....Na hili Zoezi ni endelevu...yani kila Jumatatu...Kama Mshahara vile....!!! #MCM...... #Nilikuwepo🏃

UMEONA KIFAA KIPYA CHA PETIT MAN ,JE WAMJUA NI NANI?PICHA HII HAPA

Image
Wazungu wanasema "a picture is worth a thousand words",Kupitia account yake mwenyewe ya Instagram, Petitman_Wakuache amepost picha hii akimwonyesha mwanamke mrembo ambaye ndo wanatoka naye kwa sasa. post hiyo imesindikizwa kwa ujumbe huu " Yes....just two of us.....and inshallah good news are coming"

MANCHESTER UNITED WATENGA PAUNI MILIONI 100 KWA DI MARIA

Image
Angel Di Maria. KLABU ya Manchester United imetenga kitita cha pauni milioni 100 kwa ajili ya usajili na mshahara wa winga wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Argentina, Angel Di Maria. Daley Blind. Daley Blind. Pauni milioni 50 zinatarajiwa kutumika kumsajili staa huyo wa Real Madrid huku mshahara wake kwa wiki ukitarajiwa kuwa pauni 200,000. Kocha wa United, Louis van Gaal amemtaka Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Ed Woodward kumsajili Di Maria kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Marcos Rojo. Maamuzi hayo yamekuja baada ya timu hiyo kuanza vibaya Ligi Kuu ya England 'Premiership' kwa kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Swansea juzi Jumamosi. Mbali na Di Maria, United pia wanawawinda wachezaji Daley Blind wa Ajax na Marcos Rojo kutoka Sporting Lisbon. chanzo:globalpublisher.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU YAPO HAPA

Image