Posts

HIKI HAPA KIONJO CHA VIDEO MPYA YA PROFESSOR JAY- KIPI SIJASIKIA (TEASER))

Korea yasimamisha safari kuingia Kenya

Shirika la ndege la Korea limepiga marufuku safari zake za ndege kuingia nchini Kenya kufuatia tahadhari ya shirika la afya duniani WHO kuwa taifa hilo liko katika hadhari ya kuambukizwa homa ya Ebola. Japo hakujakuwa na maambukizi yeyote ya Ebola nchini Kenya shirika la ndege la Kenya linafunga safari katika mataifa ya Magharibi mwa Afrika yaliyoathirika na Ebola. Aidha uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta ni kitovu cha usafiri wa ndege katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati. Shirika hilo linashikilia kuwa usafiri huo kutoka Magharibi mwa Afrika hadi Nairobi ndiyo changamoto inayoweza kuleta maambukizi mapya ya Ugonja huo. Chanzo:bbc swahili.

UKAWA WAZIDI KUITESA CCM NA VICHWA VINGINE VYA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS, AGOSTI 21 YAPO HAPA

Image

MARCOS ROJO ATIMKIA MANCHESTER UNITED

Image
Marcos Rojo amewasili England kwa ajili ya kukamilisha usajili wake Manchester United. KLABU ya Manchester United imekubali kutoa Pauni Milioni 16 kumnunua beki wa Sporting Lisbon, Marcos Rojo. Rojo, ambaye ametua mjini Manchester na kusema kuhamia United 'anahisi kama ndoto', anatarajiwa kusaini Mkataba wa miaka minne akifaulu vipimo vya afya na kukubali vipengele binafsi vya kandarasi yake. Louis van Gaal ametoa kipaumbele kwa usajili wa beki huyo mtumia mguu wa kushoto, Rojo, mwenye umri wa miaka 24, kufuatia kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England Jumamois na Swansea. Winga Luis Nani, aliyejiunga na United kutoka Sporting kwa Pauni Milioni 17 mwaka 2007, amerejeshwa kwa mkopo klabu yake hiyo ya zamani, ilia ni sehemu ya dili hilo la Rojo.

VIDEO MPYA YA NICKI MINAJ "ANACONDA" YAFIKISHA WATAZAMAJI 5,856,035 KABLA YA SIKU KUISHA

Image
Video ya music inayoendelea kushikilia record kutoka youtube ni ya PSY ya "Gangnam style" ambayo mpaka sasa ina zaidi ya watazamaji 2,066,230,670 tangu ilipotoka December 21,2012 . Video hii mpya ya Nicki Minaj " Anaconda" uwenda ikavunja record hiyo, video hii imekuwa gumzo kote duniani hasa kwa wapenzi wa muziki, Je ni nini haswa kimefanya video hii iweze kutazamwa zaidi na kufikisha watazamaji 5,856,035 mara baada ya kuwekwa ikiwa haijamaliza hata siku moja tangu kuwekwa kwake kwenye account yake ya vevo ya youtube?. Lugha iliyotumika sio nzuri kabisa lakini utata mkubwa uko katika mavazi yaliyotumika kwa upande wa akina dada wanaoonekana katika video hii na Nicki Minaj mwenyewe alivyo vaa na kutingisha booty.

PICHA KALI NNE ZA UTATA KATI YA NICKI MINAJ NA RAPPER DRAKE KUTOKA KATIKA VIDEO YA "ANACONDA"

Image
Nicki Minaj kupitia account yake ya instagram  amepost baadhi ya picha zilizochukuliwa katika utengenezaji wa video yake ya Anaconda inayotarajiwa kuachiwa kesho Jumatano 20/8/2014 kupitia account yake ya VEVO ya Youtube.  Rapper Drake ameonekana kwenye video hii iliyotayarishwa na Colin Tilley. Nicki Minaj atafanya show ya Mtv Video Music Awards na huu wimbo wake mpya kutoka kwenye album ya The Pink Print.

VIDEO: TIZAMA VIDEO TEASER YA NEY WA MITEGO -"MR. NAY"