Korea yasimamisha safari kuingia Kenya

Shirika la ndege la Korea limepiga marufuku safari zake za ndege kuingia nchini Kenya kufuatia tahadhari ya shirika la afya duniani WHO kuwa taifa hilo liko katika hadhari ya kuambukizwa homa ya Ebola.

Japo hakujakuwa na maambukizi yeyote ya Ebola nchini Kenya shirika la ndege la Kenya linafunga safari katika mataifa ya Magharibi mwa Afrika yaliyoathirika na Ebola.
Aidha uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta ni kitovu cha usafiri wa ndege katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati.

Shirika hilo linashikilia kuwa usafiri huo kutoka Magharibi mwa Afrika hadi Nairobi ndiyo changamoto inayoweza kuleta maambukizi mapya ya Ugonja huo.

Chanzo:bbc swahili.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA