Posts

Ebola:Wahudumu wengine washambuliwa

Image
Shirikisho la kimataifa la msalaba mwekundu, limesema kuwa kikundi kingine cha wahudumu wa afya kilishambuliwa Jumanne Kusini Mashariki mwa Guinea walipokuwa wanakusanya miili ya watu waliofariki kutokana na Ebola. Mfanyakazi mmoja wa shirika hilo, anauguza majeraha baada ya kujeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo katika eneo la Forecariah. Kulingana na mkazi mmoja, jamaa wa wagonjwa waliofariiki walianza kuwashambulia wafanyakazi hao sita wa kujitolea , na kuharibu magari yao pamoja na kuwashambulia kwa mawe wafanyakazi hao. Huu ni uvamizi wa hivi karibuni dhidi ya wahudumu wa afya ambao bila shaka unatatiza juhudi za kupambana na ugonjwa huo mkali. Wiki jana madaktari wengine na wandishi wa habari walishambuliwa Magharibi mwa nchi hiyo. chanzo; bbc swahili

Ndoa Ya Amber Rose Na Wiz Khalifa Yafikia Kikomo.

Image
  Tmz wameripoti kuwa model Amber Rose ameomba talaka kutoka kwa mume wake ambaye wameishi pamoja kwa muda  wa mwaka moja. Amber anasema yeye na mumewe wametengana kuanzia Jumatatu na anataka haki zote za malezi za mtoto wao Sebastian mwenye umri wa mwaka mmoja. Tofauti na ndoa za wasanii wengine zikivunjika hugawana pesa na mali, Amber alisainishwa makubaliano ya kutochukua mgao wa pesa au mali kutoka kwa mumewake endapo watatengana.

MKAZI WA JIJI LA MWANZA ( ROCK CITY ) KAA MKAO WA KULA NI TAREHE 04/10/214

Image

TARIBU KWELI KUTUA KENYA OCTOBER

Image
Talib Kweli, rapa wa kimataifa kutoka Marekani anatarajia kutua nchini Kenya tarehe 23 mwezi Octoba ambapo atakuwa DJ mshereheshaji katika tukio kubwa la kiburudani huko Westlands Nairobi. msanii wa nchini Marekani Talib Kweli Rapa huyu kupitia ukurasa wake wa Twitter amewatangazia mashabiki wake Afrika Mashariki juu ya ujio wake huu mkubwa, katika ziara ambayo ataianzia Afrika Kusini tarehe 3 mwezi Octoba. Ujio wa supastaa huyu nchini Kenya, unatangulia ule wa rapa 2 Chainz ambaye naye atatua kuzikonga nyoyo za wapenda burudani mwezi wa 11 mwaka huu.

DIAMOND AMTOA MACHOZI MENINAH

Image
Hivi karibuni Meninah na Diamond walizua na bado wanaendelea kuzua mjadala kila kukicha… Stori: Andrew Carlos YALE madai kuwa sexy lady wa Bongo Fleva aliyeibukia kwenye Shindano la Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star Search 2012, Meninah Abdulkareem ya kutaka kuolewa na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ yamemtoa machozi mwanadada huyo. Sexy lady wa Bongo Fleva aliyeibukia kwenye Shindano la Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star Search 2012, Meninah Abdulkareem. Hivi karibuni Meninah na Diamond walizua na bado wanaendelea kuzua mjadala kila kukicha ambapo taarifa juu ya wawili hao kutaka kufunga ndoa ya chinichini zinaendelea kusambaa kwa fujo ambapo mwanadada huyo amelonga na Amani kwa dakika kumi. TUJIUNGE NA CHANZO Kikizungumza kwa kujiamini, chanzo makini ambacho kiliomba hifadhi ya jina kilidai kwamba hakuna ndoa tena kati ya Diamond na Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na kwamba ndoa inayopangwa kwa sasa ni ya Meninah na Diamond

MAGAZETI YA ALHAMIS, SEPTEMBER 25 YAPO HAPA

Image

ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015

Bofya jina la chuo kupakua faili lenye orodha ya majina ya waliochaguliwa BUGANDO BScN_2014.pdf  (82.4 KB) BUGANDO MD.pdf  (106.2 KB) BUGANDO MEDICAL LABORATORY SCIENCES.pdf  (79.7 KB) BUGANDO PHARMACY.pdf  (80.0 KB) BUGANDO NURSING.pdf  (76.0 KB) IFM BACHELOR DEGREE 2014 MAKUMIRA PROPOSED STUDENTS 2014/2015 MUM Undergraduate Selection - Direct.pdf (561.3 KB) MUM Undergraduate Selection - Equivalent.pdf (202.0 KB) SAUT Selected Students.pdf (307.3 KB) ST. AUGUSTINE 2014 ST Franscis MD Batch one  (52.3 KB) ST Franscis MD Batch two  (37.2 KB) ST Franscis MD Batch Three  (49.5 KB) Stella Maris Mtwara.pdf  (283.1 KB) UDSM 2014/2015

TANGAZO LA KAZI SSRA DEADLINE OCTOBER 7

 DOWNLOAD ATTACHMENT HII KUONA NAFASI HIZO. FILE LIPO KATIKA MFUMO WA PDF click hapa

Picha: Amber Rose ashare picha yake ya utupu Instagram kabla ya Hackers kuzitoa

Image
  Wakati mastaa wengine wanahaha baada ya picha zao za utupu kuvujishwa mtandao bila ridhaa zao, stripper wa zamani na mke wa rapper Wiz Khalifa, Amber Rose ameamua kutowasubiri hackers wafanye mambo, kwa kuamua kuvujisha mwenyewe picha yake ya utupu kupitia akaunti yake ya Instagram.

AJALI YA NOAH YAUA WAWILI MBEYA

Image
Gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T162 BXM iliyopata ajali jana maeneo ya Igurusi mkoani Mbeya. Gari hiyo ikiwa imeharibika vibaya baada ya ajali. GARI ndogo aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T162 BXM limepata ajali na kuua watu wawili jana eneo la Igurusi mkoani Mbeya. Ajali hiyo ilitokea majira ya saa tatu na nusu asubuhi huko Igurusi kilometa 45 kutoka Mbeya Mjini na kuua dereva aliyefahamika kwa jina moja la Rashid na mama mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika. chanzo:globalpublishers.

MWENDESHA BAJAJ AJERUHIWA KATIKA AJALI TEGETA

Image
Dereva wa Bajaj iliyogongwa na Coaster eneo la Tegeta jana akiwa na majeraha mkononi. Bajaj ikiwa imeharibika vibaya baada ya kugongwa na Coaster. AJALI hii imetokea jana eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam ikilihusisha daladala aina ya Toyota  Coaster lililokuwa likiendeshwa kwa mwendo kasi na kuigonga Bajaj ambapo dereva wa Bajaj na mpiga debe mmoja aliyekuwa eneo hilo wote  walijeruhiwa. chanzo:globalpublishers.

KATUNI YA LEO

Image