AJALI YA NOAH YAUA WAWILI MBEYA

Gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T162 BXM iliyopata ajali jana maeneo ya Igurusi mkoani Mbeya. Gari hiyo ikiwa imeharibika vibaya baada ya ajali.
GARI ndogo aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T162 BXM limepata ajali na kuua watu wawili jana eneo la Igurusi mkoani Mbeya.
Ajali hiyo ilitokea majira ya saa tatu na nusu asubuhi huko Igurusi kilometa 45 kutoka Mbeya Mjini na kuua dereva aliyefahamika kwa jina moja la Rashid na mama mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika.

chanzo:globalpublishers.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA