TARIBU KWELI KUTUA KENYA OCTOBER

Talib Kweli, rapa wa kimataifa kutoka Marekani anatarajia kutua nchini Kenya tarehe 23 mwezi Octoba ambapo atakuwa DJ mshereheshaji katika tukio kubwa la kiburudani huko Westlands Nairobi.
msanii wa nchini Marekani Talib Kweli
Rapa huyu kupitia ukurasa wake wa Twitter amewatangazia mashabiki wake Afrika Mashariki juu ya ujio wake huu mkubwa, katika ziara ambayo ataianzia Afrika Kusini tarehe 3 mwezi Octoba.
Ujio wa supastaa huyu nchini Kenya, unatangulia ule wa rapa 2 Chainz ambaye naye atatua kuzikonga nyoyo za wapenda burudani mwezi wa 11 mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA