Andrew Nyerere; Mwalimu angekuwepo angepinga ufisadi!
Kuna maswala kadha wa kadha yanayoikabili Tanzania kwa hivi sasa, miongoni mwa mambo haya ni sakata la akaunti ya Tegeta/Escrow, mchakato wa katiba mpya na mengine mengi. Mwandishi Nova Kambota amefanya mahojiano na Andrew Julius Nyerere ambaye ni mtoto wa kwanza wa baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere, fuatana naye katika mahojiano haya……………… SWALI; Kuna mambo kadhaa yaliyojitokeza siku za karibuni ambayo watu wanataka kufahamu manufaa yake kwa taifa, moja ya matukio hayo ni ziara ya Jafar Mermo Idd Amin mtoto wa rais wa zamani wa Uganda marehemu Idd Amin mwaka 2008, je ziara hiyo ambayo ilimkutanisha na Madaraka Nyerere walipozuru Butiama ilikuwa na manufaa gani kwa taifa? JIBU; Kwa familia ya Mwalimu Nyerere na familia ya marehemu Idd Amin nadhani ilikuwa jambo zuri kuleta upatanishi, kuhusu kama taifa lilipata faida sijui. Aliongea Jafari kuhusu kuanzisha mfuko wa hela kuwasaidia wanajeshi walioathirika na vita vya Kagera(wa Uganda na Tanzania), pia nch