Posts

CLUB MPYA YA MAISHA BASEMENT ZAMANI NEW MAISHA CLUB KUZINDULIWA SIKU YA IDD MOSI ,

Image
  Mratibu wa Burudani wa Club mpya ya ‘Maisha Basement’ zamani New Club Maisha, Hemed Kavu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu uzinduzi wa Club hiyo utakaofanyika Idd Mosi katika Jengo la LAPF Towers lililopo mkabala na Makumbusho ya Taifa eneo la Kijitonyama ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda. Kulia ni Meneja Mkuu wa Club hiyo, Allan Ngugi na Meneja Uendeshaji wa Sam Kaliuki.    Mratibu wa Burudani wa Club mpya ya ‘Maisha Basement’ zamani New Club Maisha, Hemed Kavu (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Meneja wa Matukio, Robert Salehe na Kulia ni Meneja wa Burudani, Geofrey Gilla.   Meneja wa Burudani, Geofrey Gilla, akiwaonesha wanahabari ukumbi huo.   Meneja Mkuu wa Club hiyo, Allan Ngugi  (kulia), akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Club hiyo,Jean Claud Ciza wakati wa utambulisho wa uzinduzi huo kwa wanahabari.   Mtaalamu w

DC MAKONDA AKUTANA NA VIJANA WASIO NA AJIRA NA KUWAUNGANISHA, KUBUNI MIRADI YA KIUCHUMI ILI KUPUNGUZA TATIZO LA AJIRA

Image
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akizungumza na vijana  ambao hawana ajira  wenye elimu tofauti  katika viwanja vya Leaders  jijini Dar es salaam, ambapo amekutana na vijana hao  ili kuzungumza nao kwa ajili ya kutatua tatizo lao lao la ajira . DC Makonda amesema lengo la kuwaita vijana hao ilikuwa ni kuwakutanisha  wafahamiane na wabadilishane mawasiliano lakini pia wataunda vikundi vyao kulingana na taaluma zao na kila kundi litaandika miradi ipatayo mitano ili tuweze kuifanyia kazi kwa kuwatafutia mitaji au ufadhili baada ya miradi yao kubuniwa  Ameongeza kwamba mpango huu utapunguza vijana kukaa bila kazi na kuingia katika vishawishi vya mimba kwa wasichana na na matukio yasiyo mema katika jamii. kama vile uhalifu na mengine mengi. Lakini pia amesema kuna makampuni mengi yameahidi kuchukua vijana wenye uwezo wa kufanya kazi kwani kwa kuwaunganisha vijana hao litakuwa ni jambo rahisi kupata wafanyakazi wa kuajiri , ikiwa ni pamoja na kuchuku

EDWARD LOWASSA AKWATWA

Image
“Anakatwa, hakatwi” ndilo swali lililokuwa linaulizwa nchi nzima jana, lakini hatimaye Kamati Kuu ya CCM iliyokutana hadi usiku wa manane iliibuka na jibu kwamba Edward Lowassa amekatwa, huku kukiwa na wingu zito baada ya wajumbe watatu kupingana na uamuzi huo. Muda mfupi baada ya kikao hicho, pamoja na kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alikataa kutaja majina yaliyopitishwa, akaunti ya Twitter ya CCM, iliwataja waliopitishwa kuwa ni Bernard Membe, Dk John Magufuli, Dk Asha Rose Migiro, January Makamba na Amina Salum Ali na kuwatupa wengine 33 akiwamo Lowassa. “Kikao cha Kamati Kuu kimeisha salama. Kesho (leo) Halmashauri Kuu itakutana kuanzia saa 4:00 asubuhi,” alisema Nape baada ya kikao hicho. Alipotakiwa kutaja majina ya makada watano waliopitishwa, Nape alisema: “Nimeambiwa mchakato bado unaendelea na kesho (leo) Halmashauri Kuu itakutana kuendelea na kazi. Kwa hiyo nawakaribisha kesho kuanzia saa 4:00 asubuhi mje mchukue picha, habari, karibu sana.” Mkuta

MAGAZETI YA LEO IJUMAA

Image
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

NAPE: HAKUNA NAFASI YA KUKATA RUFAA MAJINA YAKIKATWA

Image
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwa wanachama wa chama hicho walioomba ridhaa ya chama kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya Urais iwapo majina yao yatakatwa. Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Nape Nnauye alipokutana na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya ratiba ya vikao vya mchujo wa wagombea utakaoanza siku mbili zijazo. Kikao hicho kitaongozwa na Katibu Mkuu CCM Abdulrahaman Kinana pamoja na kikao cha sekretarieti ya chama. Nape alisema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwasababu, kwanza hakuna kanuni hiyo na pia hakutakuwa na muda wa kutosha kufanya hivyo. “Tuwe wakweli tu, muda wenyewe siuoni na kanuni haisemi habari ya kukata rufaa...uchujaji wa majini kikao hakitakiwi kutoa sababu, sasa unakataje rufaa,” alisema Nape. Hata hivyo Nape amewapa matumaini wanachama wa chama hicho kuwa watatoka kwa umoja hata baada ya kupatikana kwa mgombea urais kupitia c