DC MAKONDA AKUTANA NA VIJANA WASIO NA AJIRA NA KUWAUNGANISHA, KUBUNI MIRADI YA KIUCHUMI ILI KUPUNGUZA TATIZO LA AJIRA
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh.
Paul Makonda akizungumza na vijana ambao hawana ajira wenye elimu
tofauti katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam, ambapo
amekutana na vijana hao ili kuzungumza nao kwa ajili ya kutatua tatizo
lao lao la ajira .
DC Makonda amesema lengo la
kuwaita vijana hao ilikuwa ni kuwakutanisha wafahamiane na
wabadilishane mawasiliano lakini pia wataunda vikundi vyao kulingana na
taaluma zao na kila kundi litaandika miradi ipatayo mitano ili tuweze
kuifanyia kazi kwa kuwatafutia mitaji au ufadhili baada ya miradi yao
kubuniwa
Ameongeza kwamba mpango huu
utapunguza vijana kukaa bila kazi na kuingia katika vishawishi vya mimba
kwa wasichana na na matukio yasiyo mema katika jamii. kama vile uhalifu
na mengine mengi.
Lakini pia amesema kuna
makampuni mengi yameahidi kuchukua vijana wenye uwezo wa kufanya kazi
kwani kwa kuwaunganisha vijana hao litakuwa ni jambo rahisi kupata
wafanyakazi wa kuajiri , ikiwa ni pamoja na kuchukua vijana watakaofanya
kazi kwa kujitolea na baada ya kuonyesha uwezo kazini wao wataajiriwa
na mashirika au taasisi husika.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akizungumza na vijana hao kwenye viwanja vya Leaders
Baadhi ya vijana wakiwa katika mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh.
Paul Makonda akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari kutoka kituo
cha televisheni cha Chanel Ten.
chanzo:fullshangweblog.
Comments
Post a Comment