CLUB MPYA YA MAISHA BASEMENT ZAMANI NEW MAISHA CLUB KUZINDULIWA SIKU YA IDD MOSI ,
Mratibu
wa Burudani wa Club mpya ya ‘Maisha Basement’ zamani New Club Maisha,
Hemed Kavu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu uzinduzi wa Club hiyo utakaofanyika
Idd Mosi katika Jengo la LAPF Towers lililopo mkabala na Makumbusho ya
Taifa eneo la Kijitonyama ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda. Kulia ni Meneja Mkuu wa Club hiyo,
Allan Ngugi na Meneja Uendeshaji wa Sam Kaliuki.
Mratibu
wa Burudani wa Club mpya ya ‘Maisha Basement’ zamani New Club Maisha,
Hemed Kavu (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Meneja
wa Matukio, Robert Salehe na Kulia ni Meneja wa Burudani, Geofrey
Gilla.
Meneja wa Burudani, Geofrey Gilla, akiwaonesha wanahabari ukumbi huo.
Meneja Mkuu wa Club hiyo, Allan Ngugi (kulia),
akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Club hiyo,Jean Claud Ciza
wakati wa utambulisho wa uzinduzi huo kwa wanahabari.
Mtaalamu wa mitambo katika Clab hiyo, Mr Dong
akifanya vitu vyake.
Ukumbi huo unavyonekana kwa ndani.
Dotto Mwaibale
MKUU
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, anatarajia kuwa mgeni rasmi
katika uzinduzi wa Club mpya ya ‘Maisha Basement’. iliyopo katika Jengo
la LAPF Towers lililopo mkabala na Makumbusho ya Taifa eneo la
Kijitonyama jijini Dar es Salaam
Hafla
ya uzinduzi wa club hiyo zamani ikujulikana kama ‘New maisha Club’
utafanyika siku ya Idd Mosi katika ukumbi huo ambapo watu mbalimbali
wamealikwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Mratibu wa
Burudani wa Club hiyo, Hemed Kavu, alisema uzinduzi utafanyika kwa siku
tatu tofauti ambazo ni leo, kesho na kilele ni siku siku hiyo ya Idd
Mosi.
Alisema
club hiyo mpya ambayo ni ya kisasa inauwezo wa kuchukua watu zaidi 700
kwa wakati mmoja na imejengwa katika kiwango cha kimataifa.
“Katika
Siku hizi zote za uzinduzi kutakuwa na burudani mbalimbali…club yetu
ina vifaa vya kisasa na dance floor ya kisasa yenye uwezo wa kurusha
matukio moja kwa moja kama video na mechi na ina maegesho ya magari
hivyo kuwa na ulinzi na usalama wa kutosha kwa mali za wateja” alisema.
Alisema
hivi sasa wamekuja tofauti na walivyokuwa maisha club Masaki, kwani
burudani zao zilikuwa zinaanza Jumatano mpaka Jumapili, lakini sasa
zitaanza Jumatatu mpaka Jumatatu huku kiingilio kikiwa ni sh. 10,000 kwa
siku zote.
Akitaja
ratiba zao, alisema siku ya Jumatatu watakuwa na ‘Blue Monday nite’ kwa
ajili ya wale wanaofanya kaz mwishoni mwa wiki, Jumanne ‘Meet and Greet
nite’ huu ni usiku wa mashabiki kukutana na mastaa mbalimbali na
Jumatano ni usiku wa Figisu figisu ambapo kutakuwa na burudani zote za
Kiswahili.
“Alhamisi
ni usiku wa ukae ambao tutakuwa tunapata burudani za bendi zetu za hapa
nyumbani, Ijumaa ‘Winngle Nite’ usiku wa kupata ngoma za kisasa, RNB na
East Africa Music, Jumamosi ‘Ibiza Nite’ kutakuwa na muziki wa kihindi
na kiarabu, na Jumapili ‘Bongo Swagg’ ni usiku wa live performance kwa
wanamuziki wetu,” alisema. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Comments
Post a Comment