Wapiganaji wa IS kuondoka kusini mwa Damascus
Na RFI Nchini Syria, makubaliano yaliowashangaza wengi yamefikiwa juu ya kuondoka Jumamosi hii kwa watu 4000 katika maeneo matatu kusini mwa mji wa Damascus. Watu hao ni pamoja na wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS), wapiganaji wa kundi la Al-Nusra Front na raia wa kawaida, vyanzo vilio karibu na mazungumzo vimebaini Ijumaa Desemba 25. Hii ni mara ya kwanza kwa mkataba kama huu unaolishirikisha kundi la Islamic State. Mkataba huu unaruhusu watu 4000, ambao ni raia pamoja na wapiganaji hasa wa kundi la Islamic State na wale wa kundi la Al-Nusra Front, kuondoka katika kambi ya wakimbizi wa Palestina ya Yarmuk, k