Magufuli amalizia Baraza la Mawaziri



Picha naEast Africa Television (EATV)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza baraza la Mawaziri la kwanza katika awamu ya tano ya utawala wake
Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
1. Amemteua Profesa Jumanne Maghembe kuwa waziri wa maliasili na utalii.
2. Dk. Philip Mpango ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango
3. Dk Joyce Ndalichako ameteuliwa na kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi
4. Mhandisi Gerson Lwenge ameteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
5. Prof. Makame Mbarawa ameteuliwa kuwa waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
6. Mh. Hamad Masauni ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika Sikukuu za Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
23 Desemba, 2015

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA