Ahukumiwa kwa alichokiandika Facebook kuhusu uvamizi wa kituo cha polisi Tanzania
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Bruno Kimaryo, kifungo cha
miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kusambaza ujumbe
katika mtandao wa kijamii wa kuyapongeza majambazi yaliyovamia Kituo cha
Polisi cha Stakishari na kuua polisi. Aidha, mshtakiwa huyo ametakiwa
ama kulipa faini ya Sh. 600,000 kwa kosa hilo.
Katika tukio la Stakishari lililotokea Julai 12, mwaka huu, majambazi yalivamia kituo hicho na kuua polisi wanne na raia watatu pamoja na kupora bunduki 20 aina ya Sub Machine Gun (SMG).
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Waliarwande Lema, baada
ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi watano wa upande wa
mashtaka. Alisema vielelezo vitano na utetezi wa mshtakiwa vinaonyesha
kuwa Bruno alifurahia kitendo kilichofanywa na majambazi hao na
alitamani kila kituo cha polisi kivamiwe.
Alisema mshtakiwa huyo katika ujumbe wake huo alitumia viunganishi vya maneno yasiyokuwa ya kibinadamu ya auawe, avamiwe na kuwa utetezi wake unaungana na maelezo ya onyo aliyoyatoa polisi hayaonyeshi kusikitishwa wala kuhurumia polisi.
Hakimu Lema alisema kama mshtakiwa angekuwa anapeleka ujumbe kwa polisi wachukue tahadhari, angeupeleka katika mamlaka husika, lakini kutokana na lugha aliyoitumia, mahakama hiyo inamtia hatiani.
Hata hivyo, mshtakiwa huyo alifanikiwa kulipa faini na kukwepa adhabu ya kifungo.
Awali, ilidaiwa kuwa Julai 13, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, mshitakiwa huyo anadaiwa kusambaza machapisho ya uchochezi kinyume cha Sheria ya Magazeti kwa nia kuleta ushawishi na kueneza chuki katika mtandao wa kijamii wa Facebook.

- via NIPASHE
Comments
Post a Comment