Posts

MAGAZETI YA LEO IJUMAA, JUNE 24

Image

Kamishna Kova aagwa rasmi kustaafu kazi ya utumishi wa umma

Image
Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akipunga mkono kwa Maofisa, wakaguzi, Askari na wageni mbalimbali waliohudhururia sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi. Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake wakati wa sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi Maofisa wa Polisi wakisukuma gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova kutoka katika viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi wakati wa sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki. Gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova likipita katika ya gwaride ikiw

ELIMU KWA UMMA JUU YA MANUFAA YA MATUMIZI YA MAJINA YA KIKOA CHA DOT TZ (.TZ DOMAIN NAMES)

Image
Taarifa kwa umma kuhusu matumizi ya majina ya kikoa cha .tz TAARIFA KWA UMMA TOKA RAJISI YA DOT TZ YAH: ELIMU KWA UMMA JUU YA MANUFAA YA MATUMIZI YA MAJINA YA KIKOA CHA DOT TZ (.TZ DOMAIN NAMES) Tanzania Network Information Centre (tzNIC) au Rajisi ya dot tz ni kampuni inayoendesha na kusimamia rasilimali ya nchi (dot tz) kwa ajili mawasiliano kupitia mtandao wa Intaneti. tzNIC inapenda kuuarifu umma wa watanzania kuwa imetenga siku za Jumatatu (27 Juni 2016) na  Jumanne (28 Juni 2016) kutoa elimu kwa umma juu ya kazi zake, manufaa ya matumizi ya majina ya kikoa cha dot tz (.tz domain names) na namna bora ya kuhama kutoka matumizi ya majina mengine ya vikoa kama dot com na dot org kwenda kikoa cha dot tz. Katika kipindi hicho tzNIC pia itapokea maoni mbalimbali juu ya uboreshaji wa huduma zake na nini kifanyike ili watanzania wengi wasajili na kutumia majina ya kikoa cha dot tz kwa ajili ya biashara zao, huduma zao na matumizi binafsi. Tukio hili l

Magazeti ya Leo Alhamisi, June 23

Image

Moise Katumbi, ahukumiwa kifungo cha miaka 3 jela

Image
Mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi akiasindikizwa na wafuasi wake mahakamani, mjini Lubumbashi, Mei 11, 2016. Mahakama moja mjini Kamalondo, Lubumbashi, imemuhukumu kifungo cha miaka 3 jela, aliyekuwa gavana wa jimbo la Katanga na mgombea urais kupitia muungano wa vyama vya upinzani, Moise Katumbi Chapwe. Katumbi alishtakiwa mahakamani kwa tuhuma za kumdhulumu nyumba raia mmoja wa Ugiriki, Alexander Stoupis, tuhuma ambazo mara zote, Katumbi amekuwa akikanusha. Hukumu hii ambayo imetolewa bila ya Katumbi mwenyewe kuwepo mahakamani kutokana na kuwa nje ya nchi akiendelea kupatiwa matibabu, imeamsha hisia kali miongoni mwa wafuasi wake na vyama vya upinzani. Tayari aliyekuwa spika wa Bunge la Katanga na mmoja wa wanachama wa mu

Ajira serikalini zasitishwa

SERIKALI imesitisha ajira zote, kama njia ya kukabiliana na wimbi la watumishi hewa. Kutokana na uamuzi huo hivi sasa hakuna nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa Serikali na wakala zake pamoja na utoaji wa vibali wa likizo ya bila malipo. Akizungumza na   MTANZANIA   jana jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro, alisema kuwa Serikali imesitisha kwa muda utoaji wa ajira, ili kupitia upya muundo wa Serikali na taasisi zake. Alisema utekelezaji wa mkakati huo utakwenda sambamba na kusitisha kwa muda utoaji wa vibali vya ajira zote mbadala pamoja na uidhinishaji wa ajira hizo zilizopo Sekreterieti ya Ajira katika utumishi wa umma na kwenye mfumo wa taarifa za kiutumishi. “Ni kweli tumesitisha kwa muda ili kupitia mfumo wa Serikali na hata kuangalia ulipaji wa mishahara kama upo katika malipo stahiki. “…na hili litakwenda sambamba na hata kusitishwa malipo ya mishahara yanayotokana na upandishwaji wa vyeo kwa watumishi. Tukimaliza zoezi hili ndipo tunaweza kuanz

Tangazo la ajira ya muda ya kukusanya ushuru wa maegesho ya magari

Image

IGP MANGU -AKAGUA UJENZI WA KITUO KIPYA CHA KUPOKELEA SIMU ZA DHARURA (CALL CENTRE)

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa kituo kipya cha kupokelea simu za dharura (CallCentre) wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo  ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kitazinduliwa hivi karibuni ikiwa ni hatua mojawapo  ya utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha usalama wa Jamii, unaotekelezwa na Jeshi la Polisi kwakushirikiana na Ofisi ya Rais, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi(PDB) katika mkoa wa Kipolisi Kinondoni ambapo kupitia kituo hicho wananchi wataweza kuripoti matukio na kupokelewa mapema tofauti na ilivyo hivi sasa. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa kituo kipya cha kupokelea simu za dharura (CallCentre) wakati alipofanya

[video] Kauli ya Sumaye na Polisi walivyowatawanya wanafunzi waliokuwa kwenye mahafali Dodoma

Image
[video]Kauli ya Sumaye na Polisi walivyowatawanya wanafunzi waliokuwa kwenye mahafali Dodoma Video iliyopachikwa hapo chini inaonesha ilivyotokea leo katika ukumbi wa hoteli ya African Dream mjini Dodoma, ambapo jeshi la polisi limewatawanya wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa katika ukumbi huo kwa ajili ya kushiriki mahafali yaliyoandaliwa na viongozi wa chama hicho. Inayovuata ni video ya wanafunzi wa vyuo vikuu Dodoma waliozungumza na waandishi wa habari mara baada ya polisi kuwatawanya katika hoteli ya African Dream. Ya mwisho ni video ya alichokisema Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye leo, katika ukumbi wa hoteli ya African Dream mjini Dodoma, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya jeshi la polisi kuwatawanya wanafunzi wa vyuo vikuu waliokuwa kwenye mahafali.