Moise Katumbi, ahukumiwa kifungo cha miaka 3 jela
Mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi akiasindikizwa na wafuasi wake mahakamani, mjini Lubumbashi, Mei 11, 2016.
Mahakama
moja mjini Kamalondo, Lubumbashi, imemuhukumu kifungo cha miaka 3 jela,
aliyekuwa gavana wa jimbo la Katanga na mgombea urais kupitia muungano
wa vyama vya upinzani, Moise Katumbi Chapwe.
Katumbi
alishtakiwa mahakamani kwa tuhuma za kumdhulumu nyumba raia mmoja wa
Ugiriki, Alexander Stoupis, tuhuma ambazo mara zote, Katumbi amekuwa
akikanusha.
Hukumu
hii ambayo imetolewa bila ya Katumbi mwenyewe kuwepo mahakamani kutokana
na kuwa nje ya nchi akiendelea kupatiwa matibabu, imeamsha hisia kali
miongoni mwa wafuasi wake na vyama vya upinzani.
Tayari
aliyekuwa spika wa Bunge la Katanga na mmoja wa wanachama wa muungano wa
G7, Kyungu Wakumwanza, amekosoa hukumu hiyo akisema ni ya uonevu na
inayolenga kummaliza kisiasa, Katumbi.
Mbali na
kuhukumiwa kifungo gerezani, mahakama pia imemtaka alipe faini ya kiasi
cha dola za Marekani, milioni moja kama fidia kutokana na dhuluma
aliyoifanya.
RFI
Comments
Post a Comment