Lulu ‘kajibebisha’ kwa Diamond Platnumz amchokonoa Zari


Chanzo:GPL

UCHOKOZI! Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael 'Lulu' anatengeneza kichwa cha habari kwa mara nyingine baada ya kudaiwa ‘kujibebisha’ kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz', kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni kumchokonoa mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Tukio hilo lilijiri usiku mnene Jumapili iliyopita kwenye Ukumbi wa House Club uliopo Masaki, Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya bethdei ya DJ wa Diamond, Rommy Jones.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyeweka kambi ukumbini humo, Lulu, bila kujali kwamba, Diamond alimwacha Zari nyumbani akimnyonyesha ‘baby girl’ wao, Latifah Nasibu a.k.a ‘Princess Tiffah’, alionekana akijiachia naye kimahaba huku akionesha ‘kummisi’ kinoma jamaa huyo.
rommmmILIANZA HIVI
Lulu, alikuwa wa mwishomwisho kuingia ukumbini ambapo baada ya kuzunguka kusalimiana na mastaa wengine alitua kwenye sofa alilokuwa amekaa Diamond ambapo walianza kufanya yao bila kujali ëwavimba machoí waliokuwa wakiwakodolea.
Kwa kuwa Diamond alikuwa host (mwendeshaji) wa shughuli hiyo, Lulu alikuwa akimwaga mauno huku akimshangilia Diamond kufuatia muziki wake wa nguvu uliokuwa unarindima ukumbini humo.
Kutokana na hali hiyo, Lulu aliendelea kucheza zaidi kwa madai kwamba anaupenda mno muziki wa Diamond hasa ulipodondoshwa ule wa Mdogomdogo.
mondandzarinewWAONESHANA MAHABA
Ilifika wakati Diamond alionekana akimpiga Lulu busu mdomoni huku watu wakishangilia ëoyoooí lakini wao hawakuwa wakijali chochote kwani waliendelea kufanya yao.
Kuna wakati walikuwa wakitaniana na kucheka huku wakigongesha glasi zao za mvinyo na kukumbushana mambo mbalimbali ya siku za nyuma.
Baadhi ya watu walisikika wakisema kwamba, Lulu anamchokonoa mama Tiffah ‘Zari’ kwani kwa usiku huo yeye alikuwa tu nyumbani akinyonyesha wakati baba mtoto wake akijiachia na kimwana huyo.
“Naona Lulu anatafuta matatizo kwa Zari kwani mahaba wanayooneshana hapa ukumbini siyo ya kawaida, yaani hawa mastaa wetu mbona majangaaa,” alisikika mmoja wa wahudhuriaji wa shughuli hiyo iliyokuwa ya kistaa kwani hakukuwa na ‘watoto wa mbwa’.
SHETTA AMWAGA FEDHA
Katika sherehe hiyo ilipambwa na mastaa kibao wa fani mbalimbali na mapedeshee wa mjini, walimmwagia Rommy mvua ya fedha huku mwanamuziki, Nurdin Bilal ‘Shetta’ akimzawadia fedha taslimu Sh. milioni moja ambapo shughuli iliendelea hadi majogoo.
Wakati hayo yakitendeka mmoja wa marafiki wa karibu wa Zari alimtumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) kumfahamisha juu ya tukio hilo.
MASTAA KIBAO
Ukiacha Lulu na Shetta, baadhi ya mastaa wengine waliojiachia vya kutosha ni pamoja na Aunt Ezekiel na baba mtoto wake, Moses Iyobo, dada wa Diamond, Mwajuma Abdul ‘Queen Darleen’, Khaleed Mohamed ‘TID Mnyama’, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ sambamba na Juma Musa ‘Jux’, Hamad Ally ‘Madee’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na wengine kibao.
LULU ANASEMAJE?
Akizungumzia hali hiyo, Lulu alisema kuwa ilikuwa ni pati na kupiga picha na Diamond haikuwa ishu kubwa kwani ni watu wengi waliopiga naye picha.
“Siamini wala sihisi kama Zari anaweza ‘kumaindi’ ishu kama hiyo. Kama akimaindi atakuwa na lake jambo,” alisema Lulu.
TUJIKUMBUSHE
Kabla ya tukio hilo, Lulu aliwahi kudaiwa kutoka na Diamond lakini alikanusha vikali ishu hiyo huku akionesha kuwa jamaa huyo hana ubavu wa kumsogelea wala kufaidi penzi lake.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA