DAVIDO: SUALA LA KUOA SI LA KIPAUMBELE KWANGU


Mwanamuziki maarufu wa Nigeria, David Adeleke.
MWANAMUZIKI maarufu kijana wa Nigeria, David Adeleke ajulikanaye zaidi kama Davido, amesema hana haraka ya kuoa hivi sasa ambapo nadhari yake ameielekeza kwenye tasnia ya muziki ambayo ndiyo inampa riziki yake na kwamba hataki kujifungia katika ‘sanduku’ na ndoa.

Davido aliyesema hayo hivi karibuni katika mahojiano na gazeti la Punch ambapo aliweka wazi kwamba bado hajaamua kumuoa mama wa mtoto wake, licha ya upendo wake mkubwa ambao amekuwa akiuonyesha kwa mtoto wake.
Msanii huyo aliyeimba wimbo maarufu wa 'Skelewu' alisema: “Ni jambo jema sana kuitwa baba, lakini sifikirii kuoa sasa kwani kipaumbele changu hivi sasa ni muziki. "Hivyo, wapenzi wa mwanamuziki huyo watabidi wasubiri na kuona ni lini atafunga ‘pingu za maisha’.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA