Meninah aolewa kimyakimya jijini Dar na mtoto wa Waziri
WENYE wivu wajinyonge! Nyota wa muziki wa kizazi kipya, zao la BSS 2012 Meninah Abdulkarim, anadaiwa kufunga ndoa kimyakimya mwishoni mwa wiki iliyopita na mtu anayetajwa kulelewa tangu utotoni na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini aliyejiuzulu, Profesa Sospeter Muhongo.
Chanzo chetu makini kimearifu kuwa shughuli hiyo ilifanyika Agosti 16 mwaka huu ikimaliziwa na sherehe kubwa iliyofanywa nyumbani kwao, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
“Ebwana Meninah kaolewa na jamaa mmoja ambaye tumeambiwa ni mtoto wa Muhongo, ambaye alikuwa naye kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu sasa, ndoa hiyo ilikuwa ya siri maana sisi hatukujua kabisa, ila nilikuwa naenda zangu mjini mara nikakutana na magari ya harusi ndiyo nikajumuika na mimi kula ubwabwa,” kilisema chanzo chetu ambacho kilishuhudia shughuli nzima.
Inadaiwa kuwa bwana harusi amelelewa kwa muda mwingi wa maisha yake na Profesa Muhongo kiasi kwamba watu wa karibu na familia hiyo walifahamu ni mtoto wake wa kumzaa. Hata hivyo, haikuweza kujulikana mara moja uhusiano baina ya Profesa na bwana harusi huyo, anayedaiwa kuwa ni mfanyabiashara mzuri hapa nchini.
Gazeti hili liliwasiliana na kaka yake Meninah ambaye pia ni meneja wake, Atik Abdulkarim ambaye alikiri dada yake kufunga ndoa, lakini akashangaza baada ya kudai hafahamu jina la shemeji yake, ingawa alisema ni kweli mume ni mtu aliyelelewa na Profesa Muhongo.
“Ni kweli Meninah kaolewa jana (Jumapili), ila jina la bwana harusi mimi silijui maana nimezoea kumuita shemeji tu,” alisema Atik.
Comments
Post a Comment