Posts

TASWIRA:LOWASSA NDANI YA JIJI LA MBEYA

Image
Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Ukawa kwa tiketi ya Chadema Mhe.Edward Lowassa akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Ukawa baada ya kutua Jijini Mbeya leo kwa lengo la kujitambulisha .. Wapenzi wa Ukawa Jijini Mbeya wakati wa shamrashamra za kumpokea Mgombea Urais wa Ukawa kupitia Chadema Mhe. Edward Lowassa ambaye ametua Jijini humo leo.  Mgombea Urais wa UKAWA Kupitia CHADEMA Leo atakuwa Jijini Mbeya kwa ajili ya kutambulishwa na kusaka wadhamini. Hapa kuna picha kadhaa za shamrashamra za wananchi wakimsubiri kwa hamu kubwa uwanja wa ndege wa Songwe.

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, UMAKINI UNAHITAJIKA KATIKA KUCHAGUA KIONGOZI BORA

Image
MAANDALIZI ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka huu ni ya kipekee kutokana na kupambwa na mbwembwe nyingi ikiwamo misafara na maandamano makubwa ya wagombea urais. Ni jambo la kujivunia kuona kwamba wananchi wengi wameonyesha mwamko mkubwa wa ushabiki wa kisiasa. Hadi sasa dalili za awali zinaonyesha kwamba ushindani mkubwa wa kinyang’anyiro cha urais utakuwa kati ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Misafara na maandamano makubwa ya wagombea urais hao vinazidi kuteka akili za wananchi wengi waliogawanyika katika makundi mawili yanayoelekea kulingana; kundi linalomshabikia Lowassa na jingine linalomuunga mkono Dk. Magufuli. Kutokana na misukumo mikubwa ya hisia za kisiasa, kuna wananchi ambao ukiwambia kuwa Dk. Magufuli ndiye rais ajaye wanaweza kukutoa roho! Vivyo hivyo, wapo wengine ambao wakikusikia unasema njia ya Lowassa kuelekea

Mtoto sasa amzuzua Diamond kutwa nzima chumbani akipiga picha

Image
Kitendo cha kujaaliwa kupata mtoto wa kike, kimeonekana kumzuzua mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambapo sasa anadaiwa kushinda kutwa nzima chumbani akipiga picha za kuposti mitandaoni. Chanzo makini ambacho ni ndugu wa Diamond kimeeleza kuwa, tangu jamaa huyo aitwe Baba Tiffah, amekuwa akitumia muda mwingi na mwanaye huyo kiasi kwamba amepunguza hata kasi ya kufanya muziki na kutokula.  “Jamaa ni kama kadata vile, yaani kuna siku anashinda chumbani tu akimsaidia Zari kulea, ikiwa hivyo basi siku hiyo itakuwa ni ya kupiga picha tu za kutupia mitandaoni, kiukweli mtoto amemzuzua mshikaji,” kilidai chanzo hicho.

Shamsa, Nay, siamini kama nyie ni wa kutafuta kiki! ...suala la mapenzi, si wa muziki wala filamu

Image
  WAANDISHI wa habari na mastaa wa fani mbalimbali duniani ni watu wa familia moja. Wanakutana, wanaongea na baadhi yao wanajenga urafiki mkubwa au hata kuoana. Kuna msururu mrefu wa mastaa walioingia katika uhusiano wa kimapenzi na waandishi au kujenga urafiki wa kindugu. Ni rahisi kwangu kwa mfano, kukutana na staa yeyote mkubwa katika nchi hii kuliko inavyoweza kuwa hivyo kwa mtu mwingine. Hata kama sijawahi kukutana naye, ni kiasi cha kujitambulisha na kuomba miadi naye. Inaweza isiwe muda ule nitakao mimi, lakini mwishowe tutakutana na kufahamiana. Inakuwa rahisi kwa sababu ni watu tunaotegemeana kikazi. Mimi nitahitaji kujua habari zake ili niihabarishe jamii kama ambavyo yeye atanihitaji mimi ili nipeleke ujumbe kwa mashabiki wake. Zipo baadhi ya nyakati unakutana na msanii kwa mfano, hajui namna gani atapromoti kazi yake, iwe nyimbo au filamu, hivyo kutokana na uzoefu unaweza kumpa mwongozo wa suala hilo. Kifupi ni watu tunaoishi nao, tunajuana vizuri kiasi kwamba baadh

MAGAZETI YA LEO IJUMAA, 14 AGOST YAPO HAPA

Image
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .