Posts

AIRTEL SUPA5 MWANZA KUPAMWA NA JUMANATURE, ROMA NA MWASITI MWISHONI MWA WIKI HII VIWANJA VYA FURAHISHWA

Image
Msanii mahiri wa kundi la wanaume halisi Juma Nature akiwa sanjari na Stoper Rymes makamuzi ya tamasha maalum la kuitambulisha huduma ya airtel supa5 wakati wa tamasha maalum lililoandaliwa na Airtel mwishoni mwa wiki mkoani Arusha viwanja vya NMC. Wiki hii msanii huyu na wenzake wanatarajiwa kuhusika jijini Mwanza kwenye viwanja vya Furahisha. Mwanamuziki wa bongo fleva ya home Tz mwanadada Mwasiti akikamua kibao chake cha SOJA huku akipewa tafu ma msanii mahiri wa Hip hop maarufu kama Godzilla katika tamasha la Airtel SUPA5 hivi karibuni. Wiki hii msanii huyu anatarajiwa kufanya vitu vyake jijini Mwanza kwenye viwanja vya Furahisha. Wasanii wa kinoko (maarufu kwa comedy dance) pichani pia walitoa burudani Arusha viwanja vya NMC wiki iliyopita mwishoni mwa wiki hii wanatarajiwa kufanya mambo mazuri zaidi jijini Mwanza kwenye viwanja vya Furahisha Juma Nature, Roma na Mwasiti kufunika tamasha la Airtel SUPA5 mwishoni mwa w

WALEMAVU WATAKA UWAKILISHI TUME YA KATIBA MPYA

HABARI KUTOKA KWA MWAKILISHI WA BLOG HII KUTOKA MUSOMA  Shomari Binda Musoma Jamii ya Walemavu wasiosikia (viziwi) wameiomba Serikali kuweka wawakilishi wao katika Tume ya mchakato wa Katiba mpya ili waweze kuingiza maoni yao kwa kina mara watakapoanza kukusanya maoni juu ya upatikanaji wa Katiba mpya itakayo kuwa na tija kwao pamoja na walemavu wengine. Wito huo ulitolewa na mmoja wa walemavu hao John Ogonya alipokuwa akichangia mjadala katika mdahalo ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya Mra Development Forum kuhusu utawala bora na uwajibikaji katika mchakato wa kupata katiba mpya uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Anglican mjini hapa. Alisema Walemavu viziwi wamekuwa wamekuwa wakitengwa katika masuala mbalimbali ya kijamii na kupelekea kukosa ufahamu wa mambo kutokana na ulemavu wa kutokusikia waliokuwa nao. John alidai kuwa katiba mpya inapaswa kuwa mkombozi wao kwa kuingizwa vipengere vitakavyoweza kuwasaidia kupata wataalam

Diamond kusindikiza Miss Dar Intercollege 2012 ,Juni 22

Image
MSANII wa muziki wa kizazikipya nchini Nasib Adbdul ‘Diamond’ anatarajiwa kupamba shindano la kumsakaMiss dar Intercollege 2012 linalotarajiwa kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi waMakumbusho ya Taifa , uliopo mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail alisema jana kwamba mbali na Diamond,onyesho hilo pia litapambwa na burudani kutoka bendi ya Skylight iliyopo chini ya mshirikiwa Tusker Project Fame mwaka juzi, Anneth Kushaba. Alisema maandalizi yashindano hilo yanakwenda vema ambapo warembo 14 watakaosghiriki  wanaendelea na mazoezi katika hoteli ya  The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dares Salaam                                                    “Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmojaya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina. Warembo watakaoshirikishindano hilo  wanat

Show ya A.Y na Mwana FA ndani ya Big Brother Africa 2012

Image

MISS DAR INDIAN OCEAN 2012

Image

Taarifa: TFDA yafanya uchunguzi, yazitaja dawa bandia zilizopo sokoni, zitambue, jihadhari

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yenye jukumu la kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya ya jamii kwa kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya bidhaa hizi.  Kati ya tarehe 28 Mei na 12 Juni 2012,  TFDA ilifanya Operesheni Maalum katika maeneo mbalimbali Kanda ya Ziwa  ikiwa ni mwendelezo wa Operesheni za kubaini bidhaa duni na bandia kwenye soko kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi nchini pamoja na Ofisi za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) za mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera. Ukaguzi na upekuzi ulifanyika kwenye maduka ya dawa, kituo cha mabasi ya kwenda mikoani, nyumba za makazi ya watu, nyumba za kulala wageni na ofisi zinazojishughulisha na kuuza shajala (stationeries). Lengo la Operesheni hii lilikuwa ni kuwabaini na kuwakamata wale wote wanaojihusisha na biashara ya dawa duni na bandia kinyume cha Sheria ya Chakula, D

PIGA KURA YAKO SASA NIIBUKE MSHINDI KATIKA TUZO ZA BLOG

Image
Awali ya yote napenda kutoa shukurani zangu kwa wadau wote wa blog hii kwa kuweza kunipigia kura za kuingia katika shindano la blog bora za kitanzania kupitia Tanzanian Blog Awards,ambapo kwa mwaka huu mchakato ulikuwa mgumu sana wa kuweza kupata blog ambazo zingeingia katika categories zilizokuwa zimewekwa kwani ni zaidi ya blog 200 zilizopendekezwa,nami nimepata bahati hiyo kupitia ninyi wadau kwa kura zenu za kutosha na kuweza kuingia katika shindano hilo. Kuanzia Jumatatu kupitia shindano la kuchagua blog bora za kitanzania inayoratibiwa na website ya http://www.tanzanianblogawards.com wadau mtaanza kupiga kura zenu kwa zile blog ambazo zimeweza kupata nafasi ya kuchaguliwa  katika vipengele tofauti tofauti , blog yako hii imepata nafasi pia ya kuingia katika shindano hili katika category ya Best Family or Personal Blog. Kura zimeanza kupigwa leo jumatatu tarehe 17th June na mwisho wa kupokea kura ni tarehe 30th June, mchakato huu utafanyika kwa muda wa wiki mbili tu kupitia