WALEMAVU WATAKA UWAKILISHI TUME YA KATIBA MPYA
- Get link
- X
- Other Apps
HABARI KUTOKA KWA MWAKILISHI WA BLOG HII KUTOKA MUSOMA
Shomari Binda
Musoma
Jamii ya Walemavu wasiosikia (viziwi) wameiomba Serikali kuweka
wawakilishi wao katika Tume ya mchakato wa Katiba mpya ili waweze
kuingiza maoni yao kwa kina mara watakapoanza kukusanya maoni juu ya
upatikanaji wa Katiba mpya itakayo kuwa na tija kwao pamoja na walemavu
wengine.
Wito huo ulitolewa na mmoja wa walemavu hao John
Ogonya alipokuwa akichangia mjadala katika mdahalo ulioandaliwa na asasi
isiyo ya kiserikali ya Mra Development Forum kuhusu utawala bora na
uwajibikaji katika mchakato wa kupata katiba mpya uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Anglican mjini hapa.
Alisema Walemavu
viziwi wamekuwa wamekuwa wakitengwa katika masuala mbalimbali ya kijamii
na kupelekea kukosa ufahamu wa mambo kutokana na ulemavu wa kutokusikia
waliokuwa nao.
John alidai kuwa katiba mpya inapaswa kuwa
mkombozi wao kwa kuingizwa vipengere vitakavyoweza kuwasaidia kupata
wataalamu wa lugha za alama katika huduma mbalimbali za jamii ikiwa ni
pamoja na katika hudumaa afya,mahakama na katika ofisi mbalimbali za
umma na vyombo vya habari.
Ameeleza ushilikishwaji kwa
walemavu wasio sikia umekuwa mdogo na hata wanapoelekea katika mchakato
wa kupata katiba mpya hata ile iliyopo mpaka sasa hawaifahamu na hivyo
kukosa cha kutolea maoni bali wameomba kuwepo na uwakilishi katika
Tume ya Katiba ili aweze kuingiza maoni yao.
Hata hivyo
Walemavu walioshiriki katika mdahalo huo wameishukuru asasi ya Mara
Development Forum kwa kuandaa mdahalo huo na kuwawekea wataalamu wa
lugha za alama na kupelekea kuelewa kwa kina kile kilichokuwa
kikizungumzwa na kuchangiwa kuhusu utawala bora na uwajibikaji katika
mchakato wa kupata katiba mpya.
Akichangia katika mdahalo huo
Mratibu wa Mara Development Forum George Chibasa alisema lengo la
kuandaa Mdahalo huo ambao umekuwa ukifanyika kila Wilaya katika Mkoa wa
Mara ni kuwajengea uwezo Wananchi ili kuwa na umakini mkubwa wa kutoa
maoni yao katika mchakato wa kupata katiba mpya mara Tume ya kukusanya
maoni itakapoanza kukusanya maoni.
Mratibu huyo ameishukuru
Taasisi isiyo ya kiserikali ya The Foundation For Civil Society ya Dar
es salaam kwa kuendelea kuwapa ufadhiri ambao unawasaidia kuwafikia
Wananchi na kutoa elimu mbalimbali juu ya umuhimu wa kutoa maoni yao
katika kuelekea upatikanaji wa Katiba mpya.
Hivi karibuni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete alitangaza majina
ya wajumbe wa Tume ya kukusanya maoni juu ya upatikanaji wa Katiba mpya
itakayokuwa chini ya Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba ambayo
bado haijaanza kazi ya kukusanya maoni.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment