PIGA KURA YAKO SASA NIIBUKE MSHINDI KATIKA TUZO ZA BLOG
Awali
ya yote napenda kutoa shukurani zangu kwa wadau wote wa blog hii kwa
kuweza kunipigia kura za kuingia katika shindano la blog bora za
kitanzania kupitia Tanzanian Blog Awards,ambapo kwa mwaka huu mchakato
ulikuwa mgumu sana wa kuweza kupata blog ambazo zingeingia katika
categories zilizokuwa zimewekwa kwani ni zaidi ya blog 200
zilizopendekezwa,nami nimepata bahati hiyo kupitia ninyi wadau kwa kura
zenu za kutosha na kuweza kuingia katika shindano hilo.
Kuanzia Jumatatu kupitia shindano la kuchagua blog bora za kitanzania inayoratibiwa na website ya http://www.tanzanianblogawards.com
wadau mtaanza kupiga kura zenu kwa zile blog ambazo zimeweza kupata
nafasi ya kuchaguliwa katika vipengele tofauti tofauti , blog yako hii
imepata nafasi pia ya kuingia katika shindano hili katika category ya Best Family
or Personal Blog. Kura
zimeanza kupigwa leo jumatatu tarehe 17th June na mwisho wa
kupokea kura ni tarehe 30th June, mchakato huu utafanyika kwa muda wa
wiki mbili tu kupitia blog ya tanzanianblogawards.
Mungu awabariki sana
Comments
Post a Comment