AIRTEL SUPA5 MWANZA KUPAMWA NA JUMANATURE, ROMA NA MWASITI MWISHONI MWA WIKI HII VIWANJA VYA FURAHISHWA


Msanii mahiri wa kundi la wanaume halisi Juma Nature akiwa sanjari na Stoper Rymes makamuzi ya tamasha maalum la kuitambulisha huduma ya airtel supa5 wakati wa tamasha maalum lililoandaliwa na Airtel mwishoni mwa wiki mkoani Arusha viwanja vya NMC. Wiki hii msanii huyu na wenzake wanatarajiwa kuhusika jijini Mwanza kwenye viwanja vya Furahisha.
Mwanamuziki wa bongo fleva ya home Tz mwanadada Mwasiti akikamua kibao chake cha SOJA huku akipewa tafu ma msanii mahiri wa Hip hop maarufu kama Godzilla katika tamasha la Airtel SUPA5 hivi karibuni. Wiki hii msanii huyu anatarajiwa kufanya vitu vyake jijini Mwanza kwenye viwanja vya Furahisha.
Wasanii wa kinoko (maarufu kwa comedy dance) pichani pia walitoa burudani Arusha viwanja vya NMC wiki iliyopita mwishoni mwa wiki hii wanatarajiwa kufanya mambo mazuri zaidi jijini Mwanza kwenye viwanja vya Furahisha
Juma Nature, Roma na Mwasiti kufunika tamasha la Airtel SUPA5 mwishoni mwa wiki hii Mwanza BURE
·Tamasha kufanyika kwa siku mbili mfululizo BURE
Mchakato wa kuendelea kuitambulisha huduma ya Airtel Supa5 mikoani utaendelea mwishoni mwa wiki hii ambapo Airtel itaweka kambi mkoani Mwanza katika viwanja vya wazi vya furahisha vilivyopo jijini Mwanza.

 
Akizungumzia tamasha hilo la kuitambulisha SUPA5 mkoani Mwanza Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema lengo la kuunganisha utambulisho huu burudani ni kuwavutia vijana na wateja wengi kuhudhuria na kujifunza faida lukuki za SUPA5 ili waitumie zaidi

Tamasha linafanyika kwa siku mbili mfululuzizo ambapo siku ya jumamosi tunatoa fulsa kwa wasanii chipukizi kujitokeza kwa wingi kuonyesha vipaji vyao sambamba na kupata huduma ya Airtel SUPA5


Jumapili itakuwa uzinduzi kamili ambapo wasanii wakubwa watatoa burudani BURE, akiwemo Juma Nature na kundi zima la wanaume halisi, Mwasiti a.k.a SOJA, Roma Mkatoliki a.k.a mzee wa tuzo kibao watatoa burudani kali kwa wateja watakaohuduria tamasha hilo BURE


Bi Matinde pia amezungumzia lengo la huduma ya dili tano bomba zilizopo kwenye huduma ya SUPA5 kuwa Airtel inatimiza dhamira yake iliyojiwekea ya kufikisha na kupunguza gharama za mawasiliano nchini kote bila kuwasahau vijana na wanafunzi kunufaika kwa kupata internet bure wakati wa usiku, kutuma sms bure na faida nyingine nyingi.

Huduma ya Airtel SUPA5 ilizinduliwa rasmi siku za karibuni jijini Dar es salaam kisha kufuatiliwa na kufanyika kwa matamsaha ya burudani ya BURE katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Iringa, Arusha huku mwishoni mwa wiki hii itakuwa zamu ya wakazi wote wa Mwanza


Wasanii mahiri waliokwishapamba majukwaa ya Airtel SUPA5 hadi sasa kwa mkoa wa Dar es salaam ni Fid Q, Mwasiti, Godzilla, pamoja na Kundi la Tip Top Connection akiwemo Madii, Tundaman, Richard na Dodo Janja kwa mkoa wa IRINGA ni Juma Nature na kundi zima la wanaume halisi,Roma mkatoliki, pamoja na Kundi la Tip Top Connection akiwemo Madii, Tundaman na Richard. Mkoa wa Morogoro na Dodoma ni kundi mahiri la Wanaume family likiongozwa na Chege na Temba na kukamilisha ladha ya zaidi kwa kuwepo kwa Bendi Maarufu jijini ya Mashujaa band ikiongozwa na kingunge Charles Baba na wasanii wengine.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA