Diamond kusindikiza Miss Dar Intercollege 2012 ,Juni 22
MSANII
wa muziki wa kizazikipya nchini Nasib Adbdul ‘Diamond’ anatarajiwa
kupamba shindano la kumsakaMiss dar Intercollege 2012 linalotarajiwa
kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi waMakumbusho ya Taifa , uliopo mkabala
na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Mratibu
wa shindano hilo Dina Ismail alisema jana kwamba mbali na
Diamond,onyesho hilo pia litapambwa na burudani kutoka bendi ya Skylight
iliyopo chini ya mshirikiwa Tusker Project Fame mwaka juzi, Anneth
Kushaba.
Alisema
maandalizi yashindano hilo yanakwenda vema ambapo warembo 14
watakaosghiriki wanaendelea na mazoezi katika hoteli ya The Grand
Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dares Salaam
“Mwaka
huu tumejipanga vema kuhakikisha mmojaya warembo kutoka Miss Dar
Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema
Dina.
Warembo
watakaoshirikishindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE),
Uandishi wa Habari (DSJ) naTime, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha
(IFM) na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo tajilinashikiliwa na Rose Msuya
kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana,Blessing Ngowi alitinga
fainali za Miss Tanzania.
Dina
aliwataja warembo haokuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose
Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema
Michael,Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha
Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano
hilo limedhaminiwana kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya
Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel,ScreenMasters,Makumbush ya Taifa,Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada
Hotel,Grand Villa Hotel, SportiKizaa zaa, Clouds Fm na blog za Michuzi,
Mamapipiro, Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaana Fullshangwe.
Comments
Post a Comment