Posts

IMEKAA VIPI HII

Image
KAZI KWENU WADAU

KUTANA NA VICHWA HV NDANI YA VICTORIA FM- MUSOMA 90.6

Image
KAMA NI MARAFIKI WA UKWELI NDO HAWA WAPATE UWAPO KANDA YA ZIWA, MKOA WA MARA KATIKA MASAFA YA 90.6 NI VICTORIA FM, KUTOKA SHOTO LADY MARIA MGABO, ISABELA MSHANA , PASCHAL MICHAEL BUYAGA NA CARES ONE . NI MOTO BALAAA ! augustino picha ni kwa hisani ya blog ya www.gsengo.blogspot.com

Arusi ya Alicia Keys na Swizz Beatz ilifanyika Wikiendi

Image
Alicia Keys na Swizz Beatz Hatimaye ule uhusiano wa tangu mwaka 2008 kati ya mwanamuziki wa Marekani bi. Alicia Keys na mtayarishaji wa muziki Kasseem Dean aka Swizz Beatz umezaa ndoa mwishoni mwa wiki Alicia Keys na Swizz BeatzHafla ya ndoa hiyo ilifanyika kwa faragha kubwa siku ya Jumamosi katika eneo ambalo halijatajwa. Alicia Keys, miaka 29, amewahi kujishindia tuzo mbalimbali 12 za Grammys tangu kutoa albamu yake ya kwanza Songs in A Minor mwaka 2001. Dean, miaka 31, ambaye ana watoto wawili kutoka ndoa yake ya mwanzo, ameandika na kutayarisha nyimbo za wasanii zilizovuma sana akiwemo Beyonce na mumewe Jay-Z. Alicia Keya aliimba katika sherehe za ufunguzi za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwezi Juni, 2010.

Vigogo wazidi kubwagwa CCM

MATOKEO ya kura za maoni kwa nafasi za ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) yamezidi kutolewa nchini huku yakiwatupa nje ya bunge baadhi ya waliokuwa wakishikilia majimbo mbalimbali, jambo linaloashiria kuwa bunge lijalo litakuwa na sura nyingi mpya. Mkoa wa Dar es Salaam Katika Mkoa wa Dar es Salaam walioibuka kidedea na kuwamwaga wapinzani ni, Dkt. Makongoro Mahanga Jimbo la Segerea (2,148) akifuatiwa na Bw. Joseph Kessy (1,435), Jimbo la Ukonga aliyeoongoza katika matokeo ya awali ni Bi. Eugen Mwaiposya (1,885) akifuatiwa na Bw. Godwin Barongo (1,394), Jimbo la Kinondoni aliyeongoza ni Bw. Iddi Azan) akifuatiwa na Bi. Shy-Rose Bhanji, Jimbo la Ubungo aliyeibuka mshindi ni Bi. Hawa Ng'umbi ambaye amewamwaga Bw. Nape Mnauye na Bi. Shamsa Mwangunga. Mkoa wa Dodoma Mkoani ambao umetoa matokeo ya awali katika majimbo yote na matokeo hayo yanaweza kubadilika mara baada ya kukamilika kuhesabiwa kura katika vituo vyote. Jimbo la Dodoma Mjini Bw. Peter Chiwanga (3,183), Bw. David Mal...

CHADEMA wampitisha Mbilinyi kuwania ubunge

Image
JOSEPH MBILINYI MWANAMUZIKI wa kizazi kipya nchini, Bw. Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Mr.II jana aliibuka kidedea kuwa mgombea ubunge Jimbo la Mbeya mjini baada ya kuwashinda mhandisi wa mitambo ya simu, Bw. Daud Mponzi na mwandishi wa habari wa Tanzania Daima, Bw. Christopher Nyenyembe. Katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Kiwira Motel ulishirikisha wapiga kura 362 kutoka katika kata zote 36 wa jijini Mbeya. Mwanamuziki huyo alishinda kwa kura 175 akifutiwa na Bw. Daud Mponzi aliyepata 122, mwandishi wa habari mndawamizi wa Tanzania Daima, Bw. Christopher Nyenyembe kura 54 na mwanaharakati Gwakisa Mwakasendo aliyeambulia kura 9. Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa, Bw. Sambwee Shitambla aliwataka wanachama wa chama hicho kuhakikisha wanachagua mgombea atakayeweza kukiuza chama hicho kupambana na CCM na hatimaye kushinda jimbo hilo. Alisema kuwa chama hicho hakitaki mgombea atakayepita kwa mbinu za kifisadi kama ilivyo kwa wagombea wengi wanaodaiwa kufan...

Kocha Stars aja leo, kuanzia kibarua

KOCHA mpya wa Taifa Stars, Jan Poulsen anatua nchini leo kuanza kibarua chake kipya ambacho kitaanzia rasmi Cairo, Misri dhidi ya mabingwa wa Afrika, Mafarao, Agosti 11. Poulsen, raia wa Denmark atawasili nchini leo usiku kuinoa Stars iliyoachwa na Marcio Maximo aliyemaliza muda wake mwanzoni mwa mwezi. Kulingana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mechi hiyo ambayo ni ya kirafiki ya kimataifa ilipangwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa,Fifa. Ofisa Habari waTFF, Florian Kaijage, alisema jana kuwa baada ya kuwasili nchini Poulsen atakuwa na jukumu la kuanza mchakato wa kuteua wachezaji wa Stars na kuwaandaa kwa mechi hiyo siku kumi baadaye. Kaijage alisema kuwa ni matarajio ya shirikisho hilo kuwa mechi hiyo itakuwa sehemu muhimu ya matayarisho ya Stars kuanza harakati za kusaka tiketi ya kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika za mwaka 2012 zitakazoandaliwa kwa pamoja na Gabon na Guinea ya Ikweta. "TFF imekuwa ikifanya jitihada kubwa kuhakikisha St...

HIVI NDO ILIVYOKUWA FIESTA KUJIPANGUSA MUSOMA

Image
Hivyo ndo ilivyokuwa jana katika swala zima la kujipangusa pande za Musoma,leo watu wa Mwanza wanajipangusa leo na kesho pia......... picha hizi ni kwa hisani ya michuzijr