Arusi ya Alicia Keys na Swizz Beatz ilifanyika Wikiendi


Alicia Keys na Swizz Beatz

Hatimaye ule uhusiano wa tangu mwaka 2008 kati ya mwanamuziki wa Marekani bi. Alicia Keys na mtayarishaji wa muziki Kasseem Dean aka Swizz Beatz umezaa ndoa mwishoni mwa wiki

Alicia Keys na Swizz BeatzHafla ya ndoa hiyo ilifanyika kwa faragha kubwa siku ya Jumamosi katika eneo ambalo halijatajwa.

Alicia Keys, miaka 29, amewahi kujishindia tuzo mbalimbali 12 za Grammys tangu kutoa albamu yake ya kwanza Songs in A Minor mwaka 2001.

Dean, miaka 31, ambaye ana watoto wawili kutoka ndoa yake ya mwanzo, ameandika na kutayarisha nyimbo za wasanii zilizovuma sana akiwemo Beyonce na mumewe Jay-Z.

Alicia Keya aliimba katika sherehe za ufunguzi za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwezi Juni, 2010.


Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA