CHADEMA wampitisha Mbilinyi kuwania ubunge

JOSEPH MBILINYI

MWANAMUZIKI wa kizazi kipya nchini, Bw. Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Mr.II jana aliibuka kidedea kuwa mgombea ubunge Jimbo la Mbeya mjini baada ya kuwashinda mhandisi wa mitambo ya simu, Bw. Daud Mponzi na mwandishi wa habari wa Tanzania Daima, Bw. Christopher Nyenyembe.

Katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Kiwira Motel ulishirikisha wapiga kura 362 kutoka katika kata zote 36 wa jijini Mbeya.


Mwanamuziki huyo alishinda kwa kura 175 akifutiwa na Bw. Daud Mponzi aliyepata 122, mwandishi wa habari mndawamizi wa Tanzania Daima, Bw. Christopher Nyenyembe kura 54 na mwanaharakati Gwakisa Mwakasendo aliyeambulia kura 9.

Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa, Bw. Sambwee Shitambla aliwataka wanachama wa chama hicho kuhakikisha wanachagua mgombea atakayeweza
kukiuza chama hicho kupambana na CCM na hatimaye kushinda jimbo hilo.

Alisema kuwa chama hicho hakitaki mgombea atakayepita kwa mbinu za kifisadi kama ilivyo kwa wagombea wengi wanaodaiwa kufanya hivyo kutokana na CCM, badala yake wanataka wagombea watakaoweza kuuzika na kukipa chama ushindi wa kishindo katika ubunge, urais na udiwani.

Alionya kuwa hatakubali kumpitisha mgombea yeyote atakayefanya hila kushinda na hatimaye kukiletea aibu chama hicho, alichodai wanananchi wana imani nacho katika mapambano ya kuung’oa utawala wa chama tawala madarakani.

Awali, Bw. Mbilinyi akijinadi kwa wagombea alisema kuwa atahakikisha anajenga ofisi za chama hicho kuanzia kata hadi wilaya, ili kufanikisha azma ya CHADEMA kuongoza Jimbo la Mbeya kwa kuwa na madiwania wote kutoka chama hicho na ana imani ya kuishinda CCM.

Baada ya kutangazwa kwa matokeo wagombea wote walikubali matokeo na kuahidi kuungana na mshindi katika kuleta ushindi kwa chama hicho, kwa kuamini kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA