Vigogo wazidi kubwagwa CCM
MATOKEO ya kura za maoni kwa nafasi za ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) yamezidi kutolewa nchini huku yakiwatupa nje ya bunge baadhi ya waliokuwa wakishikilia majimbo mbalimbali, jambo linaloashiria kuwa bunge lijalo litakuwa na sura nyingi mpya.
Mkoa wa Dar es Salaam
Katika Mkoa wa Dar es Salaam walioibuka kidedea na kuwamwaga wapinzani ni, Dkt. Makongoro Mahanga Jimbo la Segerea (2,148) akifuatiwa na Bw. Joseph Kessy (1,435), Jimbo la Ukonga aliyeoongoza katika matokeo ya awali ni Bi. Eugen Mwaiposya (1,885) akifuatiwa na Bw. Godwin Barongo (1,394), Jimbo la Kinondoni aliyeongoza ni Bw. Iddi Azan) akifuatiwa na Bi. Shy-Rose Bhanji, Jimbo la Ubungo aliyeibuka mshindi ni Bi. Hawa Ng'umbi ambaye amewamwaga Bw. Nape Mnauye na Bi. Shamsa Mwangunga.
Mkoa wa Dodoma
Mkoani ambao umetoa matokeo ya awali katika majimbo yote na matokeo hayo yanaweza kubadilika mara baada ya kukamilika kuhesabiwa kura katika vituo vyote.
Jimbo la Dodoma Mjini Bw. Peter Chiwanga (3,183), Bw. David Malole (2,268) akifuatiwa na Bw. Adam Kimbisa (2,141). Jimbo la Mtera aliyeongoza ni Bw. Livingstone Lusinde (5,810) akifuatiwa na Bw. John Malecela (5,379), Jimbo la Mpwapwa Bw. Gregory Teu (7,777) akifuatiwa na Bw. George Lubeleje (4,830).
Jimbo la Kondoa Kusini Bw. Juma Nkamia (4,249) akifuatiwa na Bw. Pascal Degela (632), Jimbo la Kongwa Bw. Job Ndungai anaongoza kwa kura (8,208) na Bw. John Palingo (2,295), Jimbo la Kibakwe Bw. George Simbachawene (8,824) akifuatiwa na Bw. Agrey Galawika (2,537), Kondoa Kaskazini Zabein Mhita (6,211) akifuatiwa na Bw. Mohamed Lujuomoni (2,116) na Jimbo la Bahi anayeongoza ni Bw. Donald Mejiti (2,627) akifuatiwa na Bw. Omary Sanda (1,308).
Kutoka Singida
Mkoa wa Singida, Iramba Magharibi anaongoza Bw. Lameck Mwigulu (3,834) akifuatiwa na Bw. Juma Kilimba (3,788), Manyoni Mashariki Bw. John Chiligati (3,123) akifuatiwa na Bw. Daniel Matuka (1,702).
Tabora moto
Mkoa wa Tabora Jimbo la Urambo Mashariki aliyeshinda ni Spika Bw. Samuel Sitta (6,130) akifuatiwa na Bw. Ally Maswanya (2,432), Bw. Rostam Aziz ameshinda Igunga wakati Bw. Hussein Bashe ameibuka kidedea Nzega aliyemwangusha Bw. Lucas Selelii.
Shinyanga mgombea afa
Mkoa wa Shinyanga wabunge wawili wa zamani mkoani Shinyanga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaelekea kupoteza majimbo yao baada ya matokeo ya awali ya kura za maoni kuanza kupokelewa kutoka majimboni.
Wakati wabunge hao wakielekea kupoteza majimbo yao , mgombea mwingine aliyekuwa akigombea katika Jimbo la Maswa Magharibi, Bw. Amani Jidulamabambasi amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Wabunge wanaoelekea kupoteza majimbo yao ni pamoja na Bw. John Shibuda wa jimbo la Maswa Magharibi anayepambana na Bw. Robert Kisena, Jimbo la Shinyanga mjini, Dkt. Charles Mlingwa naye anaelekea kuangushwa na Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Shinyanga, Bw. Stephen Masele. Jimbo la Bariadi Magharibi, Bw. Andrew Chenge ameibuka mshindi, Bariadi Mashariki, Bw. Simon Matongo, Maswa Mashariki, Bw. Peter Bunyongoli na Kahama ameshinda Bw. James Lembeli.
Wengine ambao mpaka jana mchana walikuwa wakiongoza katika majimbo yao ni Bw. Suleiman Nchambi, jimbo la Kishapu, Bw. Ahmed Salum (Solwa), Bw. Salum Khamis, (Meatu), Bw. Emmanuel Luhahula (Bukombe), jimbo la Msalala alipita, Bw. Ezekiel Maige na jimbo la Kisesa Bw. Luhaga Mpina ameshinda.
Mkoani Mwanza
Mkoa wa Mwanza, Dkt. Festus Limbu amepita Magu, Bw. Charles Kitwanga (Misungwi), Bw. Sharif Mansoor (Kwimba), Bi. Getrude Mongela (Ukerewa), Dkt. Titus Kamani (Busega), Bw. William Ngeleja (Sengerema), Dkt. Charles Tizeba (Buchosa), Bw. Lawrence Masha (Nyamagana) na Bw. Antony Dialo (Ilemela).
Mkoa wa Kagera
Mkoa wa Kagera katika kura za awali zinaonesha kuwa Jimbo la Nkenge linaongozwa na Bi. Ansumpta Mushama (9,055) akifuatiwa na Dkt. Diodorus Kamala (6,184)
Jimbo la Muleba Kusini linaongozwa na Prof. Anna Tibaijuka akifuatiwa na Bw. Wilson Masilingi.
Muleba Kaskazini aliyeibuka kidedea ni Bw. Charles Mwijage (5,481) akifuatiwa na Bw. Thomas Niyegira (3,154) na Bi. Ruth Msafiri akiambulia kura (1,879).
Jimbo la Ngara Prof Feetham Banyikwa anaelekea kupoteza nafasi hiyo kutokana na kukaliwa vibaya na Bw. Deogratias Ntunkamazima ambaye anaoongoza kwa kura (3,954) na kufuatiwa na Bw. Alex Kashaza (3,838) huku Prof. Banyikwa akiambulia 2,112.
Jimbo la Biharamulo, mbunge wa sasa Bw. Oscar Mukasa alikuwa akiongoza kwa kura (5,899) akifuatiwa na Agricolas Magoho (974).
Jimbo la Karagwe mjini hadi sasa anayeoongoza ni Bw. Gozbert Blandes na kwa upande wa jimbo la Kyerwa linaongozwa na Justus Katagira.
Mkoa wa Mbeya, jimbo la Kyela, Dkt. Harisson Mwakyembe amezoa jumla ya kura 7,681 akifuatiwa na Bw. George Mwakalinga (574), huku Bw. Elius Mwanjala (512).
Yaliyojiri Mbeya
Jimbo la Mbeya Mjini, Bw. Benson Mpesya anaongoza kwa kura 5,586 akifuatiwa na Bw. Thomas Mwang’onda (3,362), Jimbo la Rungwe Mashariki Prof. Mark Mwandosya (4,240), akifuatiwa na Bw. Steven Mwakajumilo (228).
Jimbo la Rungwe Magharibi Prof. David Mwakyusa anaongoza kwa kura 6,974 akifuatiwa na Bw. Richard Kasesela (5,843) na Bw. Frank Magoba (1379).
Jimbo la Mbeya vijijini Mchungaji Luckson Mwanjale anaongoza kwa kura 7,353 huku Bw. Andrew Saile akipata kura 1,902.
Jimbo la Ileje Bw. Aliko Kibona (5,844), Bw. Ambonesigwe Mbwaga (2,200) na Bw. Godfrey Msongwe akiambulia kura (2,004) na Dkt. Harison Mwakyembe ameibuka kidedea Kyela.
Ruvuma
Mkoa wa Ruvuma Jimbo la Songea Mjini, Dkt. Emmanuel Nchimbi ametangazwa kuwa mshindi baada ya kupata kura 15,374 sawa na asilimia 88.3 akifuatiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Bw. Oliver Mhaiki aliyepata kura 2,816 sawa na 16.1%, Bw. Slimu mohamed (196), Bw. Renatus Mkinga (140).
Matokeo ya awali ya ubunge jimbo la Peramiho, Tunduru, Mbinga magharibi na Mashariki pamoja na Namtumbo yanaonesha wabunge wote wanaotetea nafasi zao wanaongoza kwa kura, ingawa bado kura zainaendelea kuhesabiwa.
Mkoa wa Geita
Waliopita ni Bw. Donald Max (Geita Mjini), Dkt. John Magufuli (Chato), Bw. Hussein Amari (Nyang'ware), Bw. Lolensia Bukwimba (Busanda).
Mkoa wa Kilimanjaro
Wakili wa kujitegemea, Bw. Cryspin Meela ameibuka mshindi kwa kura (7,162) huku Bw. Aloyce Kimaro akiambulia kura (3,194) katika Jimbo la Vunjo.
Moshi vijijini aliyeshinda ni Dkt. Cyril Chami, Mwanga Prof. Jumanne Maghembe, Rombo Bw. Basil Mramba na Siha Agrey Mwanry wameibuka washindi.
Jimbo la Moshi mjini, Bw. Buni Ramole alishinda kwa kura (1,554) huku Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoani hapa, Bw. Thomas Ngawaiya akiwa na kura (1,539).
Jimbo la Hai Bw. Fuya Kimbita alitetea nafasi yake kwa kuwashinda wapinzani wake kwa kura 3,725, akifuatiwa na Dunstan Malya 2,649.
Nako Same Magharibi Bw. David Mathayo alitetea nafasi kwa kura 14,281, akifuatiwa na John Isingo 608. Same Mashariki, Bi. Anne Kilango alishinda wapinzani kwa kura7, 514 akifuatiwa na Dkt. Michael Kadege kwa kura 1,804.
Mkoani Mtwara
Jimbo la Nachingwea Bw. Mathias Chikawe kaibuka mshindi wa kishindo ambaye amezoa kura 5,887 akifuatiwa na Bw. Albert Mnali kwa kura 3,912.
Wakongwe wamwagwa Kigoma
Mkoa wa Kigoma, wabunge watatu waliokuwa wakiiongoza majimbo ya Muhambwe, Kasulu Magharibi na Kigoma Kusini wanaelekea kumwagwa kwenye kura za maoni.
Jimbo la Kigoma Mjini, Bw. Peter Serukamba ameongoza kwa kura nyingi, Kutoka wilayani Kibondo mbunge wa jimbo hilo, Bw. Felix Kijiko ameangushwa na mfanyabiashara Bw. Jamal Tamim, Jimbo la Kasulu Bw. Daniel Nsanzugwanko anaongoza kwa kupata kura 1,560, akifuatiwa na Bw. Kafonogo Mayengo ( 625).
Jimbo la Kasulu Mjini Bw. Neka Rafael anatajwa kuongoza katika kura za awali akifuatiwa na Bw. Gidion Bunyaga.
Jimbo la Manyovu Bw. Kilontsii Mporogomyi ameangushwa na vijana na kujikuta nafasi ya tano kati ya wagombea tisa.
Mkoa wa Rukwa
Jimbo la Sumbawanga Mjini, Bw. Aeshy Hillaly ameibuka mshindi kwa kupata kura 867 akifuatiwa na Bi. Herieth Switi (155), Jimbo la Nkasi Kaskazini, Bw. Mohamed Keissy (1,557), Bw. Hiporitus Matete (1,173)
Katika jimbo la Nkasi Kusini, Bw. Desderius Mipata (719) akifuatiwa na Joseph Walingozi (348), Jimbo la Kwela Bw. Ignas Malocha anaongoza kwa kura (5,772), akifuatiwa na Meja January Kisango (1,772).
Jimbo la Kalambo Bw. Jepephat Kandege ( 5,597) akifuatiwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo
Bw. Ludovick Mwananzila ( 4,061).
Mkoa wa Tanga
Jimbo la Korogwe Mjini linaongozwa na Bw. Yusuph Nassir (2,513) akifuatiwa na Bw. Joel Bendera ambaye alikuwa ni mbunge wa jimbo hilo kwa kura (2,258).
Tanga Mjini Omari Nundu alishinda kwa kura 7,422 na Salum Kisanji akifuatia kwa kura 5,087 aliyekuwa mbunge Harith Mwapachu akiambulia kura 2,129; Lushoto Henry Shekifu alishinda kwa kura 4,178 akifuatiwa na Abdi Mshangaza aliyepata 2, 450.
Jimbo la Bumbuli aliyeshinda ni january makamba kwa kura 14, 612 huku mbunge aliyemaliza muda, William Shellukindo aliyepata 1,700; wakati Muheza aliyeshinda ni Herbert Mntangi kwa kura 9, 142 dhidi ya Julius Semwaiko aliyepaya kura 6, 595.
Mkoani pwani
Waliobwaga na majimbo yao kwenye mabano ni Dkt. Ibrahimu Msabaha (Kibaha Vijijini), Dkt. Zainabu Gama (Kibaha mjini), Prof. Idrisa Mtulya (Rufiji) na Bw. Ramadhani
Maneno (Chalinze).
Waliopeta ni katika kinyang'anyilo hicho ni Dkt. Shukuru Kawambwa (Bagamoyo), Bw. Adamu Malima (Mkuranga), Bw. Abdul Malombwa (Kibiti) na Bw. Abdulkarim Shah (Mafia).
Wapya waliong’ara ni Bw. Silvesta Koka (Kibaha mjini), Bw. Hamidu Abuu (Kibaha Vijijini), Bw. Said Bwanamdogo (Chalinze), Bw. Seleman Jafo (Kisarawe) na Dkt. Seif (Rufiji).
Taarifa hii ni kutoka gazeti la majira

Comments
Post a Comment